Aliyekuwa
Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahimu Lipumba alirejea nchini jana jioni
akitokea Kigali, Rwanda alikokwenda mara tu baada ya kujiuzulu wadhifa
huo siku nane zilizopita.
Profesa
Lipumba aliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius
Nyerere (JNIA) saa 10.10 jioni kwa ndege ya Rwanda Air.
Akihojiwa
na Azam Tv kwa simu akiwa Kigali, siku tatu baada ya kuondoka nchini,
Profesa Lipumba alisema alikuwa nchini humo akifanya utafiti kuona namna
gani Tanzania inaweza kujifunza mambo ya kiuchumi kutokana na nchi hiyo
kupiga hatua kubwa katika sekta hiyo.
Alipoulizwa
jana, Profesa Lipumba alisema akiwa huko alikuwa na mazungumzo na Bodi
ya Maendeleo ya Rwanda (RDB), wadau wa masuala ya rushwa, waziri wa
fedha wa nchi hiyo na makamu mwenyekiti wa Bodi ya Utawala.
“Wenzetu
wamepiga hatua kubwa katika kukuza uchumi ndani ya kipindi kifupi,
hivyo safari yangu ilikuwa ya kujifunza mbinu walizotumia kufikia
malengo yao,” alisema.
Akizungumzia
hatima yake kisiasa, licha ya kusema ataendelea kuwa mwanachama wa CUF,
alisema hatashiriki kufanya kampeni kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi
(Ukawa) kwa kuwa umoja huo umemsimamisha mwanachana wa CCM, Edward
Lowassa.
“Kisiasa
hatima yangu ni kama ya Mtanzania mwingine yeyote, Ukawa tuna mgombea
kutoka CCM, amehama juzi tu, pia mle ndani ya Bunge la Katiba hakuunga
mkongo Rasimu ya Katiba na ndiyo maana nikasema dhamira yangu inanisuta,” alisema Profesa Lipumba.
Alisema wanachama wa CUF hawana sababu ya kuona kama amewaacha kwa kuwa bado yupo nchini.
Awali,
akitangaza kujiuzulu, nguli huyo wa uchumi, alisema alifikia uamuzi huo
kutokana na Ukawa kumkaribisha Lowassa kugombea urais kupitia umoja
huo, hivyo dhamira yake inamsuta.
Mpekuzi
No comments:
Post a Comment