Ikiwa ni wiki amabayo ya Malaria
Duniani, Mataifa mbaliombali Duniani hutumia nafasi hii kufanya shughuli
mbali mbali katika kuadhimisha wiki na siku ya Malaria duniani.
Kampuni ya Bima ya AAR imetembelea
Hospitali ya Amana iliyoko Ilala Dar es salaam na kutoa msaada wa
vyandarau kwa wamama wajawazito katika kutimiza lengo la kupunguza
uenezi wa gonjwa la Malaria.
Akiongea na wandishi Habari
Hospitalini hapo, Afisa Mahusiano wa kampuni ya bima ya AAR, Bibi Amisa
Juma alisesema, “Tukiwa kama wadau wa Afya Tanzania, ni jukum letu
katika jamii kuonyesha mfano wa kupambana na maradhi mbalimbali ikiwemo
hili Malaria.
Hii imakua ni utamaduni kwa kampuni
ya Bima ya AAR kuadhimisha siku ya Malaria Duniani kwa kushirikiani na
Jamii katika shughuli mbali ikiwemo kuchangia kutoa elimu juu ya
kujikinga na tiba pamoja na kuchangia matibabu kwa jamii tofauti ya
Tanzania. Almalizia Bibi Amisa.
Wafanyakazi wa AAR walitembelea hodi ya kina na mama wajawazito na watoto na kutoa msaada huo.
|
April 27, 2016
BIMA YA AFYA YA AAR YAADHIMISHA SIKU YA MALARIA DUNIANI HOSPITALINI AMANA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment