KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

April 13, 2016

ETHADI YAPEWA TUZO KA HUDUMA BORA ZA USAFIRI WA ANGA

A11V0109
Shirika la Ndege la Etihad limepokea tuzo  ya  uzinduzi bora katika sekta ya usafiri wa ndege kwa mwaka 2016 kutoka kwenye jarida la kimataifa linaloongoza kwa makala za usafiri wa anga. Sherehe za tuzo hizo zilifanyika katika maonyesho ya ndege yaliyofanyika jijini Hamburg, nchini Ujerumani.
Shirika lilijinyakulia tuzo hiyo kwa kuzingatia viwango vya juu vya teknolojia na maendeleo ya burudani inayotolewa ndani ya ndege (E-BOX) pamoja na mtandao wa mawasiliano (IFEC) zinazopatikana kwenye safari zake za kimataifa. Tuzo hii ni muedelezo wa tuzo ambazo shirika limekuwa linajinyakulia kwa mwaka uliopitia kupitia huduma zake bora za ndani ya ndege zikiwemo, tuzo ya shirika bora la ndege mwaka 2015 kutoka jarida la Inflight, tuzo ya uzinduzi bora mpya kwa shirika la ndege mwaka 2016 kutoka jarida la kimataifa la PAX kwa kanda ya mashariki ya kati, pamoja na tuzo ya shirika lenye huduma bora za burudani ndani ya ndege kutoka jarida la World Travel.
Shane O’Hare, Makamu wa Rais kitengo cha Masoko wa Shirika la ndege Etihad, alisema: ” Tuzo hii, iliyopigiwa kura na wasomaji wa jarida la kimataifa la PAX kwa kipindi cha miezi sita, ni utambuzi tosha juu ya dhamira ya shirika la ndege Etihad  kuhakikisha wageni wetu wanaendelea kufurahia burudani bora ndani ya ndege pamoja na mtandao thabiti wa mawasiliano ndani ya ndege zetu.”
Shirika la ndege Ethihad linamiliki idadi kubwa ya ndege aina ya Airbus za kisasa pamoja na Boeing kubwa za kubeba abiria/mizigo kwa wingi na ndogo ze abiria/mizigo kidogo.
Huduma ya Tv zenye kurusha matangazo na vipindi moja kwa moja  hupatikana kwenye ndege kubwa za Shirika la ndege, hii ni kuleta vipindi bora kutoka vituo saba ikiwa ni pamoja na BBC World News, Sport 24 na CNN, zikiwa zinaongoza kwa utazamajia, na CNBC, euronews , Japan NHK World Premium na Sky News Arabia.
A11V0188

No comments:

Post a Comment