KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA NCHINI AFUNGA RASMI MAFUNZO YA MAAFISA WATEULE DARAJA LA KWANZA , MKOANI MOROGORO
Kamishna
Jenerali wa Magereza nchini, CGP John Casmir Minja akikagua Gadi Maalum
iliyoandaliwa na Maofisa Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wateule Daraja
la Kwanza yalifanyika Aprili 27, 2016 katika Viwanja vya chuo cha Jeshi
la Magereza, KPF Mkoani Morogoro.
Kamishna
Jenerali wa Magereza nchini, CGP John Casmir Minja katika jukwaa
akipokea salaam ya heshima kutoka Gadi Maalum iliyoandaliwa na Maofisa
Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wateule Daraja la Kwanza(hawapo pichani).
Maofisa
Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wateule Daraja la Kwanza wakipita mbele
ya Mgeni rasmi katika sherehe za kufunga mafunzo hayo yaliyofanyika
Viwanja vya chuo cha Jeshi la Magereza, KPF Mkoani Morogoro.
Kamishna
Jenerali wa Magereza nchini, CGP John Casmir Minja(kushoto) akimvisha
cheo cha RSM mmoja wa Wahitimu wa Mafunzo ya Maafisa Wateule Daraja la
Kwanza ambaye amefanya vizuri zaidi katika Mafunzo hayo yaliyofanyika
kwa muda wa miezi miwili.
No comments:
Post a Comment