KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

April 5, 2016

RUTO ASUBIRI UAMUZI MUHIMU

Ruto
Bw Ruto anataka kesi dhidi yake iondolewe
Makamu wa Rais wa Kenya William Ruto atafahamu leo iwapo kesi inayomkabili katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) itatupiliwa mbali.
Mwanahabari Joshua arap Sang, aliyeshtakiwa pamoja na Bw Ruto, pia atafahamu leo iwapo ana kesi ya kujibu.
Bw Ruto anakabiliwa na mashtaka ya mauaji, kuhamisha watu kwa lazima na mateso yaliyotekelezwa wakati wa vita vya baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007.
Amekana mashtaka hayo na mawakili wake wanataka kesi hiyo itupiliwe mbali kutokana na ukosefu wa ushahidi.
Watu takriban 1,200 waliuawa wakati wa mapigano hayo.
Upande wa mashtaka umekabiliwa na changamoto kadha kwenye kesi hiyo dhidi yake.
Mwezi Februari, majaji katika mahakama hiyo waliizuia afisi ya mwendesha mashtaka kutumia ushahidi wa mashahidi ambao tayari wamejiondoa.
Mashahidi kadha muhimu walibadilisha taarifa zao za ushahidi, jambo ambalo waendesha mashtaka wanasema lilitokana na vitisho na kuhongwa.
Mawakili wa Bw Ruto wanasema anafaa kuondolewa kesi hiyo kwa sababu mashahidi wengi wa upande wa mashtaka wamejiondoa au wakabadilisha taarifa zao asili za ushahidi.
  • Ruto ashinda rufaa mahakama ya ICC
  • Mashahidi wa Ruto katika ICC
  • Bensouda:Sikabiliwi na shinikizo zozote
Mwendesha mashtaka mkuu wa ICC Fatou Bensouda amekiri kwamba kujiondoa kwa mashahidi kumeathiri kesi dhidi ya naibu huyo wa rais lakini anasisitiza kwamba bado kuna ushahidi wa kutosha wa kuendelea na kesi hiyo.  BBC

No comments:

Post a Comment