KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

April 13, 2016

SUPER STAR RAY ATUHUMIWA UCHAWI,AIBUKA NA KUJIBU,AFUNGUKA MENGI MAZITO



Staa wa filamu za Kibongo, Vincent Kigosi ‘Ray’.
Na Waandishi Wetu, RISASI mchanganyiko
DAR ES SALAAM: Staa wa filamu za Kibongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ ameingia kwenye kashfa nzito baada ya kudaiwa kutumia ndumba kwenye sanaa ili kuwa juu ya wenzake, Risasi Mchanganyiko limetonywa.


Chanzo kutoka Bongo Muvi kilieleza madai kwamba msanii huyo mwenye jina kubwa, amekuwa ‘akiwachezea’ wenzake ili wasifanye vizuri kwenye soko la sanaa na sasa hivi ndiye anayeongoza kwa mauzo katika Kampuni ya Steps Entertainments baada ya Steven Kanumba kufariki dunia akifuatiwa kwa karibu sana na Stephen Jacob ‘JB’.
Inadaiwa kuwa moja ya viashiria vya ‘ulozi’ huo ni tukio la hivi karibuni lililotokea huko Kigamboni, ambapo tangazo lililowekwa ili kutangaza ujio wa filamu mpya ya JB, kupasuka muda mfupi tu baada ya kuwekwa.
“JB alienda kuweka bango la filamu yake ya Chungu cha Tatu maeneo ya Kigamboni lakini muda mfupi tu likapasuka katikati, lakini alipokuja kuweka Ray la kwake la Tajiri Mfupi lipo mpaka leo, hali imetutisha sana sisi wasanii,” kilisema chanzo hicho.
Stephen Jacob ‘JB’.
Baada ya kuzinyaka habari hizo, gazeti hili lilimtafuta Ray ili kujibu tuhuma hizo ambapo alisema: “Siamini kwenye mambo ya ushirikina, ninachoamini ni kujituma kwenye kazi na ndiyo sababu kazi zangu zinakubalika kuliko za wengine, kwani natumia gharama nyingi kuandaa kazi zangu pamoja na kutumia vifaa vyenye ubora wa juu ndiyo sababu zinafunika.
“Kuhusu bango la JB kupasuka sina taarifa hizo labda ni kutokana na hali ya hewa tu watu waachane na imani potofu.”
Hata hivyo, aliwataka mastaa wengine kuachana na maneno na kufuata nyayo zake za kufanya kazi zenye ubora kwani ndiyo siri ya mafanikio yake na si vinginevyo.
Kwa upande wa JB alipoulizwa alisema bango kupasuka siyo uchawi na hakuna kitu kama hicho.
“Mimi ni mtu mzima sasa hivi ninayejiheshimu, haya mambo unayoniuliza ni ya kitoto naomba uachane nayo tafadhali,” alisema JB

No comments:

Post a Comment