Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (katikati) akijadiliana jambo na Katibu
Mkuu wa Wizara hiyo Sekta ya Ujenzi Eng. Joseph Nyamhanga (kushoto) na
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Eng. Patrick
Mfugale wakati akikagua Daraja la Rusumo wilayani Ngara.
Muonekano wa barabara ya Nyakahura-Rusumo inayounganisha Tanzania na Rwanda kupitia Daraja la Rusumo wilayani Ngara.
Mtaalam kutoka Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA), wa pili kulia akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (wa tatu kulia),
alipotembelea ofisi hizo katika Kituo cha pamoja cha forodha (One Stop Border Post)
upande wa Tanzania kilichopo Rusumo wilayani Ngara, wa kwanza kushoto
ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Sekta ya Ujenzi Eng. Joseph Nyamhanga.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akitoa ufafanuzi kwa Mtendaji Mkuu wa
Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Eng. Patrick Mfugale (mwenye
kofia) wakati akikagua maandalizi ya ufunguzi wa Daraja la Rusumo na
Vituo vya pamoja vya forodha (One Stop Border Post) wilayani Ngara.
Muonekano wa Daraja la Rusumo
linalounganisha Tanzania na Rwanda, kushoto ni daraja la zamani lenye
rangi ya njano na kulia ni daraja jipya.
Meneja wa Kituo cha pamoja cha forodha(One Stop Border Post),
katika mpaka wa Tanzania na Rwanda upande wa Rwanda Bw. Moses Kalisa
akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof.
Makame Mbarawa na ujumbe wake walipotembelea kituo hicho.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
No comments:
Post a Comment