KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

June 3, 2016

KATIBU MKUU WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI AKAGUA MRADI WA UJENZI WA NYUMBA ZA ASKARI, NA KITUO CHA POLISI KUNDUCHI, OYSTERBAY POLISI NA MIKOCHENI JIJINI DAR ES SALAAM LEO

N1
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Meja Jenerali Projest Rwegasira (wa tatu kutoka kushoto) akielekea kukagua miradi ya ujenzi wa nyumba za polisi zilizopo katika eneo la Kunduchi jijini Dar es Salaam jana, wanne kutoka kushoto ni Bw. Bernard Chagula ambaye ndiye Msimamizi Mkuu  wa Mradi huo anayesimamia kwa niaba ya Jeshi la Polisi. 
N2
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi  Jenerali Projest Rwegasira (wa kwanza kutoka kulia) akionyeshwa mchoro wa ramani ya jengo mojawapo linaloendelea kujengwa  huko Kunduchi jiji Dar es salaam kwa ajili ya nyumba za kuishi askari wa jeshi la polisi,(wa pili  kutoka kulia) ni Bw. Bernard Chagula ambaye ndiye Msimamizi Mkuu  wa Mradi huo anayesimamia kwa niaba ya Jeshi la Polisi.
N4
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi  Jenerali Projest Rwegasira aliyenyosha mkono akitoa maelekezo kwa Jeshi la Polisi juu ya miradi hiyo inayoendelea kujengwa, wanaomsikiliza ni baadhi ya viongozi wa Jeshi la Polisi na wakandarasi wanaotekeleza mradi huo eneo la Kunduchi jijini Dar es Salaam.
N5
Bw. Bernard Chagula (wa nne kutoka kushoto) ambaye ndiye Msimamizi Mkuu  wa Miradi ya ujenzi wa nyumba za polisi anayesimamia kwa niaba ya Jeshi la Polisi, akimuonyesha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi  Jenerali Projest Rwegasira(wa pili kutoka kulia) baadhi ya majengo(hayapo pichani) yanayoendelea kujengwa katika eneo la Polisi Oysterbay jiji Dar es salaam ambapo Katibu Mkuu huyo alifanya ukaguzi kujionea maendeleo yaliyofikiwa tangu kuanza kwa mradi huo.
N3
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi  Jenerali Projest Rwegasira (watatu kutoka kushoto) akiwa pamoja na baadhi ya viongozi wa Jeshi la Polisi na wakandarasi wanaotekeleza mradi huo eneo la Mikocheni jijini Dar es Salaam, nyuma yao ni baadhi ya majengo yaliyokwisha kujengwa.

No comments:

Post a Comment