KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

June 2, 2016

MKOA WA ARUSHA KUAZIMISHA SIKU YA MAZINGIRA KWA UPANDAJI MITI JUNE 5

images
MKOA wa Arusha, utaadhimisha siku ya mazingira duniani June 5 kwa kupanda miti aina mbalimbali ya matunda ,vivuli na ya asili kwenye shule za msingi na vyanzo vya maji ili kutunza na kuhifadhi mazingira.
Katibu tawala mkoa wa Arusha,Richard Kwitega, amesema kwenye maadhimisho hayo ambayo kilele chake kitakuwa ni Juni 5 mwaka huu mkoa utapanda miti kwenye maeneo yote ya mkoa huo lengo ni kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na kutekeleza jukumu la  shirika la mazingira duniani, UNEP.
Amesema shirika la umoja wa mataifa la mazingira UNEP, limepanga juni 5 kila mwaka ni siku ya maadhimisho ya mazingira duniani,ili watu wajue umuhimu wa kutunza na kusimamia mazingira yao.
Alisema kila nchi mwanachama ikiwemo Tanzania, inayo sauti katika kikao cha baraza la mazingira duniani  juu ya mazingira endelevu .
Kwitega,alisema mwaka huu 2016 maadhimisho ya mazingira kimataifa yanaadhimishwa nchini Angola,yakiwa na kauli mbiu isemayo uvumilivu  ufike mwisho juu ya biashara haramu ya wanyama pori ambayo hupelekea wanyama pori kutoweka kwenye IKolojia.
Alisema kaulimbiu hiyo inatutaka kuacha kuwauwa wanyamapori  kwa lengo la kuuza viungo vyao  na kuharibu mazingira .
Kwitega,amesema katika kutekeleza jukumu hilo mkoa huo, unashirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo zikiwemo halmashauri na asasi binafsi kuadhimisha siku hiyo ya mzngira duniani kwa kupanda miti maeneo mbalimbali.
Alisema kwa kuanza mkoa utapanda miti ya matunda kwenye shule tano za msingi za jijini Arusha, ambazo ni Makumbushi, Arusha school, Naura, Meru na Levolosi,na kwenye chanzo cha maji cha Kiranyi, kutapandwa miti ya asili  ambayo ni rafiki wa mazingira ili kutunza chanzo hicho.
Alisema maadhimisho hay mwaka huu hayataadhimishwa kitaifa bali kila mkoa kila mkoa umepewa jukumu la kuadimisha maadhimisho hayo kwa kushirikiana na halmashauri zake na wadau wake wa maendeleo.
Alisema kauli mbiu ya taifa mwaka huu inasema tuhifadhi vyanzo  vya maji  kwa uhai wa taifa  letu  na mkoa utaendelea kutoa elimu ya uhifadhi wa mazingira kwa jamii kuanzia juni 2 hadi siku ya kilele juni 5
Kwitega, alisema  katika maadhimisho hayo wananchi na wadau watafanya usafi kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo soko la Kilombero, na kwenye makazi kuanzia ngazi ya kaya ,kitongoji,kijiji,mtaa na kata ,na akatoa wito kwa kila mwananch na taasisi mbalimbali kuhakikisha wanapanda miti kwenye maeneo yao.
Alisema kuwa siku ya kilele ya maadhimisho hayo ya mazingira duniani,mkuu wa mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda,(KIJIKO)ataongoza wananchi kupanda mti wa kumbukumbu kwenye bustani ya Peace Park, iliyopo mzunguko wa Impala hotel jijini hapa .

No comments:

Post a Comment