Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango juzi alibanwa bungeni baada
ya wabunge kutaka maelezo ya kina ya sababu za Serikali kushindwa
kuwasilisha muswada wa kurekebisha Sheria ya Manunuzi ambao
unalalamikiwa kuwa unachochea ufisadi.
Sheria hiyo imekuwa
ikilalamikiwa na wadau, wakiongozwa na Rais John Magufuli, kuwa inatoa
mwanya kwa wazabuni kupandisha bei za bidhaa wanapopewa mikataba ya
Serikali kwa kushirikiana na watumishi wa umma.
Rais Magufuli
alilalamikia sheria hiyo kwa mara ya kwanza Novemba mwaka jana wakati
akizindua Bunge, akisema inaumiza Serikali na hivyo itafanyiwa
marekebisho.
Juzi, wabunge wa CCM walisimama kidete wakimtaka
waziri huyo kuwa na majibu yanayoridhisha na kueleza kuwa asipofanya
hivyo, wangekwamisha bajeti yake, ambayo hata hivyo ilipita.
Akichangia
hotuba ya Wizara ya Fedha, Mashimba Ndaki alisema Sheria ya Manunuzi
imekuwa ikisababisha kero kubwa kwa wananchi na kuwasababishia usumbufu
usiokuwa na maana.
Ndaki
alisema sheria hiyo haifai, lakini inashangaza kuona Serikali imekuwa
kimya. Janeth Mbene alisema haiwezekani kuendelea kufumbia macho jambo
hilo tena.
Mbene
alisema pamoja na udhaifu wa sheria hiyo, Serikali inatakiwa kuangalia
upya kwa kuwa yako mashirika mengi ambayo ni mzigo hivyo akaomba
yaondolewe na kufutwa.
Mbunge wa Mpwapwa, George Lubeleje
alisema sheria ya manunuzi ni mchwa unaotafuna kila mali za umma, lakini
Serikali inaonekana kufumbia macho.
"Mimi nimekuwa mjumbe wa
bodi ya mashirika mbalimbali, lakini utakuta vitu vinavyonunuliwa na
watu moja kwa moja, bei inakuwa chini lakini kwa kupitia bei ya Sheria
ya Manunuzi inauwa mara mbili yake, huu ni wizi,” alisema Lubeleje.
Mbunge wa viti maalumu (CCM), Ritha Kabati alisema sheria hiyo imekuwa ikiwanyima nafasi wazalendo.
|
June 3, 2016
MUSWADA WA MANUNUZI WAMTOA JASHO WAZIRI WA FEDHA BUNGENI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment