VIJANA
wenye sifa za kujiunga na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), kwa
mujibu wa sheria wamekuwa wengi kiasi cha kuifanya Serikali kushindwa
kuwachukua wote, Bunge limeelezwa.
Hivyo,
kutokana na sababu hiyo, Serikali imeamua kuongeza idadi ya kambi za
mafunzo ili wachukuliwe wote. Hayo yalisemwa bungeni jana mjini hapa na
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi wakati
akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalumu, Munira Mustafa Khatib
(CCM) aliyetaka kufahamu ni kwa nini Serikali isianzishe mpango maalumu
wa kuwapeleka JKT vijana wanaomaliza kidato cha nne.
Akijibu
swali hilo, Waziri Mwinyi alisema, “Uwezo wa JKT kwa sasa kuchukua
vijana wa kujitolea ni kati ya vijana 5,000 hadi 7,000 kwa mwaka
kutokana na bajeti inayotolewa.
Alisema,
utaratibu wa sasa wa vijana kujiunga na JKT ni ule wa kujitolea kwa
vijana wenye elimu ya kuanzia shule ya msingi hadi vyuo vikuu na ule wa
mujibu wa sheria unaowahusu waliomaliza kidato cha sita.
“Kuwachukua vijana wote wanaomaliza kidato cha nne kama anavyoshauri mbunge hautowezekana kutokana na uwezo mdogo kifedha,” alisema.
Hata
hivyo, alisema ushauri huo ni mzuri na serikali itafanya maandalizi ya
kambi nyingi zaidi na kutenga bajeti kubwa zaidi kwa ajili ya uendeshaji
kwa kadri uwezo wa kifedha utakavyoruhusu.
|
June 2, 2016
SERIKALI YAZIDIWA MZIGO WA VIJANA WANAOTAKIWA KUJIUNGA JKT
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment