Afisa
Bismas Asenga mwakilishi wa Ubalozi wa Tanzania hapa Marekani akiongea
mbele ya watu waliojitokeza ndani ya kanisa kwa ajili ya Ibada ya misa
na kuaga mwili wa Andrew Nicky Sanga. Afisa Bismas ndiye aliyemwakiliza
Balozi Wilson Masilingi.
……………………………………………………………………………….
Uongozi wa Tanzania Houston
Community (THC) unapenda kukanusha taarifa zisizo sahihi zinazosambazwa
mitandaoni ya kwamba Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani chini ya Mh.
Balozi Wilson Masilingi haukufanya lolote wakati Jumuiya yetu ilipopatwa
na misiba miwili ya Bw.Henry Kiherile na Bw.Andrew Nicky Sanga
iliyotokea kwa nyakati tofauti mapema mwezi April mwaka huu.
Uongozi wa THC unapenda umma
utambue kwamba tulipata na tunathamini sana ushirikiano ulioonyeshwa na
kutolewa na Ubalozi pamoja na Balozi mwenyewe Mh. Masilingi wakati wa
misiba hiyo miwili na hata baada ya shughuli hizo za misiba kumalizika.
Baadhi ya mambo yaliyofanywa na
Balozi ni kuwatafuta viongozi wa JumuiyaTHC na kuzungumza nao mapema
baada ya misiba hiyo kutokea (Balozi alitutafuta viongozi na si
vinginevyo) ambapo alizungumza na Rais wa Jumuiya Bw.Daudi Mayocha kwa
simu na Katibu Mkuu wa Jumuiya Bw.Michael Ndejembi na kuwapa pole kwa
niaba ya familia na Jumuiya nzima.
Uongozi unafahamu kwamba sababu
za balozi kushindwa kufika Houston wakati wa misiba hiyo ni yeye
kumuwakilisha Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. John
Magufuli kwenye kongamano la DICOTA lililokuwa likifanyika jijini
Dallas, Texas. Tunatambua pia kwamba nia ya Balozi kuja Houston bado iko
pale pale.
Aidha Balozi Masilingi alimtuma
afisa Ubalozi Bismas Asenga kumuwakilisha katika shughuli za Misa na
Kuaga mwili wa marehemu Andrew Nicky Sanga, ambapo afisa huyo pamoja na
mambo mengine alitoa salamu za rambirambi toka kwa Balozi na alikabidhi
rambirambi ya $500 kwa kila familia pamoja na kuzungumza na wafiwa hao
kwa nyakati tofauti.
Kwa taratibu za kiupelelezi
Uongozi wa THC hauwezi kutoa taarifa zaidi ya namna suala hili
linavyoshughulikiwa kati ya vyombo vya usalama nikimaanisha HPD Homicide
Department na Ubalozi wa Tanzania lakini tunatambua kwamba Ubalozi
unafuatilia kesi zote mbili kwa ukaribu sana.
Uongozi wa THC unasisitiza kuwa hauhusiki kwa aina yoyote na Waraka (Petition)unaosambazwa kwenye mitandao.
kumchafua Balozi Masilingi na Ubalozi wetu wa Washington D.C kwa ujumla.
Daudi Mayocha,
Rais wa Jumuiya ya Watanzania Houston (THC)
|
June 2, 2016
TAARIFA KWA UMMA KUTOKA JUMUIYA YA WATANZANIA HOUSTON (THC)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment