Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Bw Hassan Bendeyeko akifungua kikao kati ya wadau wa Sekta za Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo na Wizara husika kilichofanyika Mjini Songea Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel na kulia ni Afisa Elimu MkoaBw.Gharama Kinderu |
Katibu Mkuu Wizara ya
Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo akisikiliza maelezo ya baadhi ya
vifaa vilivyotumika katika vita ya Majimaji kutoka kwa Afisa Elimu
Makumbusho ya Taifa Bi. Blantina Raphael wakati alipotembelea
makumbusho hayo mjini Songea, katikati ni Afisa Elimu wa Mkoa wa Ruvuma
Bw.Gharama Kinderu. picha na Zawadi Msalla- WHUSM Ruvuma
………………………………………………………………………………..
Na Zawadi Msalla- WHUSM Ruvuma
Katibu Mkuu wa Wizara ya
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel ametoa wito
kwa viongozi na wadau wa sekta ya Utamaduni wa Mkoa wa Ruvuma kutangaza
Utamaduni na Utalii unaopatikana katika mkoa huo.
Wito huo umetolewa jana mjini
Songea na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo
Prof. Elisante Ole Gabriel alipokuwa akizungumza na wadau wa sekta za
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo katika ofisi za mkuu wa Mkoa wa
Ruvuma.
“Mkoa wenu una vivutio vingi vya
asili vinavyoonesha tamaduni za wanaruvuma ambavyo vikitumika vizuri ni
fursa nzuri ya mapato” alisema Prof Gabriel.
Ameongeza kuwa Mkoa wa Ruvuma una
vivutio vingi vya Utamaduni vya kuvutia watalii ambavyo ni fursa nzuri
ya kutangaza Utamaduni wa Mkoa na Tanzania kwa ujumla.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa
Mkoa wa Ruvuma Bw.Hassan Bendeyeko alikiri kuwepo kwa changamoto ya
kuvitangaza vivutio hivyo kutokana na ubovu wa miundombinu iliyopo .
Hata hivyo alisema kuwa ujenzi
wa miundombinu utasaidia vivutio hivyo kufikika kwa urahisi na
wanategemea Mkoa huo kuinuka kiuchumi hasa baada ya changamoto hiyo
kutatuliwa.
Bw.Bendeyeko alisema kuwa baadhi
ya vivutio vya kiutamaduni vinavyo hitaji kutangazwa ili vifahamike
ndani na nje ya nchi ni pamoja na Makumbusho ya Majimaji, eneo
waliponyongwa wapiganaji wa vita vya majimaji, Ziwa Nyasa pamoja na
mbuga mbali mbali.
Aidha alieleza kuwa wanatarajia
kuajiri Maafisa Utamaduni wakutosha katika kila Halmashauri ambapo kwa
kushirikiana na Maafisa Habari na waandishi wa habari kutangaza vivutio
hivyo.
|
No comments:
Post a Comment