SHIRIKA
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), limeeleza kuridhishwa kwake na
utendaji wa Rais John Magufuli katika mapambano ya rushwa, kuongeza
uwajibikaji na ukusanyaji wa mapato.
Mwakilishi
Mkazi wa UNDP nchini, Alvaro Rodriguez, alisema hayo jana katika semina
ya wabunge kuhusu Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu ya Dunia.
Alisema
Serikali ya Awamu ya Tano, imekuwa ikipambana na rushwa na kusimamia
kwa karibu ukusanyaji mapato, hali aliyosema itasaidia maendeleo kwa
kuwa hakuna nchi iliyoendelea bila kuchapakazi.
Rodriguez
alisema mbali na kuona maendeleo katika baadhi ya mikoa na mitaa,
ameona jitihada hizo za Serikali na amefurahishwa na kuridhika nazo.
Mwakilishi
huyo pia alisema Serikali ya Tanzania na Ofisi ya Umoja wa Mataifa
(UN), zimekuwa zikifanya kazi pamoja katika harakati za usambazaji wa
malengo ya dunia kwa Watanzania.
Alisisitiza
umuhimu wa malengo hayo kueleweka kwa wabunge, ili katika jukumu lao la
kuisimamia Serikali, wawe mabalozi wa utekelezaji wa malengo hayo
katika ufuatiliaji kwenye ngazi zote za utawala.
Awali
akifungua semina hiyo, Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson aliwataka
wabunge kuoanisha malengo hayo na malengo ya Dira ya Taifa ya 2025
pamoja na malengo ya Mpango wa Taifa wa Miaka Mitano wa 2016/2017 mpaka
2020/2021 ambao ulishafikishwa bungeni.
Dk
Tulia aliwataka wabunge kila mmoja kuyaelewa vizuri malengo hayo ili
kila mmoja ashikilie mahali atakapofuatilia Serikalini wakati wa
utekelezaji wake.
Miongoni
mwa malengo hayo ni pamoja na kutokomeza umasikini wa kila aina, kufuta
njaa kwa kuhakikisha kuna kuwa na uhakika wa chakula bora kwakuboresha
kilimo endelevu, kuhakikisha watu wote wanakuwa na afya bora nakupata
huduma za afya na kupunguza utofauti wa kipato.
Akitoa
mada katika semina hiyo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na
Mipango, Paul Kessy, alisema Tanzania imeshiriki kwa kiasi kikubwa
katika maandalizi ya malengo hayo na hivyo mchango wake kuwa sehemu ya
maudhui ya malengo hayo endelevu kwa maslahi mapana ya taifa na watu
wake.
Kwa
mujibu wa Kessy, sehemu ya mchango wa Tanzania katika kuunda malengo
hayo, ilikuwa ni kutaka malengo hayo yahakikishe kuwa baadhi ya masuala
ambayo hayakukamilika katika utekelezaji wa Malengo ya Milenia
yanazingatiwa katika malengo endelevu.
Baadhi
ya mambo hayo ni pamoja na kupunguza umasikini, upatikanaji wa ajira na
kukuza uwezo wa nchi masikini hasa katika maendeleo ya teknolojia
No comments:
Post a Comment