Wabunge
saba wa upinzani waliosimamishwa bungeni, watakumbana na kibano kingine
cha kukatwa mshahara na posho kwa kipindi chote cha kutumikia adhabu.
Wabunge
hao ambao Jumatatu walisimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge kwa muda
tofauti kwa madai ya kukiuka kanuni ni Zitto Kabwe (Kigoma Mjini), Tundu
Lissu (Singida Mashariki), Halima Mdee (Kawe), Ester Bulaya (Bunda
Mjini), John Heche (Tarime Vijijini) na Godbless Lema (Arusha Mjini).
Adhabu
hiyo ilitolewa kama azimio la Bunge baada ya Kamati ya Haki, Maadili
na Madaraka ya Bunge kupendekeza wabunge hao waadhibiwe kutokana na
kuomba mwongozo wa kiti cha Spika kwa jambo ambalo tayari lilishatolewa
uamuzi.
Habari
zilizopatikana bungeni zilieleza kuwa wabunge hao watakumbana na Kanuni
ya Bunge ya 75, ambayo inahusika na masharti ya mbunge aliyesimamishwa
kazi.
Naibu
Katibu wa Bunge (Shughuli za Bunge), John Joel alithibitisha kuwa
utekelezwaji wa kanuni hiyo utafuatwa kwa wabunge wote ambao
wamefukuzwa.
Akizungumzia
hatua hiyo, Heche alisema hadi sasa hajapata barua ya kusimamishwa
Bunge, hivyo hata kama watakata posho au mshahara haimsumbui kwa kuwa
hawezi kusikitikia kitu hicho wakati haki inaminywa.
Zitto
alisema hajasikia taarifa hizo za kukatwa mshahara kwa kuwa hajapewa
barua inayoeleza mambo hayo wala ya kusimamishwa Bunge.
|
June 2, 2016
WABUNGE 7 WA UPINZANI WALIOSIMAMISHWA KUHUDHURIA VIKAO VYA BUNGE WAONGEZEWA ADHABU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment