Na Masanja Mabula –Pemba
WACHUUZI wa samaki katika
soko la Bandarini Wete , wamegoma kurejea ndani ya soko hilo wakiutaka
uongozi wa Baraza la Mji Wete kuhakikisha unarejesha huduma muhimu ndani
ya soko hilo ikiwemo maji pamoja na vyoo.
Wamesema kwamba uwamuzi wa
kutoka na kuanza kuuza samaki nje ya soko ni kutokana na kuharibika kwa
miundo mbinu ya maji ndani ya soko , jambo ambalo linahatarisha usalama
wa maisha yao na wateja wanaokwenda kupata mahitaji ya kila siku .
Wakizungumza na kamati ya
kusimami mwendendo wa wachuuzi wa samaki iliyoundwa na Mkuu wa Wilaya
ya Wete , walisema hawako tayari kurejea ndani ya soko hilo , hadi
uongozi wa Baraza la Mji utakapojipanga kurejesha huduma muhimu za
kijamii .
Mwenyekiti wa Kamati ya wavuvi
ambaye pia ni dalali wa samaki sokoni hapo Mohamed Kombo alisema endapo
huduma hizo zitarejeshwa ndani ya soko hilo , wachuuzi wote watarejea
na kuuza samaki wao kwani watakuwa na usalama wa maisha yao .
“Uongozi wa Baraza unmekusudia
kutudhalilisha , hili sio soko , maji hakuna na vyoo hakuna isiotoshe
lipo chini yam nada unafikiri nani atakayekuja kununua sakami kwa
mchuuzi wakati mnada uko hapa hapa ? ”alihaoji .
Naye Hossein Sharif Mchuuzi wa
samaki na dalali , alisema uwamuzi wa kuhama kuuza samaki ndani ya soko
ni kuwapunguzia kazi wanafanyakazi wanaosafisha ndani ya soko , kwani
wanapata usumbufu kufuata huduma kwa kichwa kwa ajili ya kusafisha baada
aya saa za kazi .
Alisema awali Uongozi wa Baraza
ulifanikisha kuunganisha huduma ya maji kwa muda , lakini huduma hiyo
ilidumu kwa muda wa wiki mbili na kukatwa , kuacha soko likiwa katika
hali tete hasa kipindi hichi cha magonjwa ya mripuko .
Kwa upande wake Khatib Said
Kombo aliiambia kamati hiyo kwamba vyoo vipo mbali na soko na haviko
katika hali nzuri , hivyo ni vyema kuangaliwa upya na kufanyiwa
marekebisho ili viweze kutumika .
Akijibu malalamiko hayo
Mkurugenzi wa Baraza la Mji Wete , Mgeni Othman Juma alisema baadhi ya
sababu zilizotolewa na wachuuzi hao sio za msingi na kwamba ambazo ni za
msingi aliahidi kuzipatia ufumbuzi wa haraka .
“Tayari uongozi wa Baraza
umelipa fedha kwa mamlaka ya Maji (ZAWA) Wilaya ya Wete kwa ajili ya
kurejesha huduma hiyo ndani ya soko , na huduma hii itarejea ndani ya
kipindi cha wiki moja , lakini wakati tunasubiri hilo kufanikishwa
tunawaomba wachuuzi warejea ndani ya soko ”alisisitiza.
Hata hivyo uchunguzi uliofanywa
na mwandishi wa habari hizi umebaini kwamba Mamlaka ya Maji Zanzibar
(ZAWA) Wilaya hiyo ilifikia uwamuzi wa kuikata huduma ya maji katika
soko hilo kwa kuwa yalikuwa hayatumiki na yalisababisha miundo mbinu
kupasuka baada ya kuzidiwa na presha yake
|
June 3, 2016
WACHUUZI WA SAMAKI WETE BANDARINI WAGOMA KUREJEA NDANI YA SOKO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment