KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

July 20, 2016

GREEN HOPE YAKABIDHI MADAWATI 100 KATIKA MKOA WA ARUSHA

ARUSHA
Mahmoud Ahmad Arusha
…………………………………………
Shirika lisilo la kiserikali la Green Hope Organization lenye makao yake jijini Arusha leo imekabidhi madawati 100 yaliotengenezwa kwa teknolojia ya kisasa inayotokana na mabaki ya chupa ya maji na mifuko ya plastiki
Akikabidhi madawati hayo kwa mkuu wa mkoa Arusha Felex Ntibenda maarufu kwa jina la kijiko mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo Emmanuel Makongoro amesema madawati hayo yametengenezwa kutokana na mabaki ya chupa tupu za maji na mifuko ya plastiki
Amesema madawati hayo yatengenezwa  kutokana na agizo la Mh Rais John Pombe Magufuli , la kuhakikisha kuwa hakuna watoto wanao kaa nchini kutokana na ukosefu wa madawati
Amesema gharama ya dawati moja ni sh.80,000, ambapo wanakusudia kutengeneza madawati  3000 ambayo watakabidhi mkoa Arusha kwa lengo la kusambaza wilaya zake
Makongoro,amesema teknolojia hiyo ya kutengeneza madawati na meza kwa kutumia mabaki ya chupa tupu  na plastiki inakusudia kutoa ajira kwa vijana ambao watakuwa wakiuza  chupa hizo  kwa sh.1500 kwa kila kilomoja.
Ameongeza kuwa  wako kwenye mikakati ya kufungua vituo vya ukusanyaji wa chupa hizo kwenye jiji la  Arusha
Amesema shirika hilo linatekeleza mradi huo wa madawati kutokana na ufadhili wa shirika la misaada la Canada (cida)Amesema shirika hilo limefungua ofisi jijini Mwanza kwa ajili ya kukusanyia chupa na mifuko ya plasiti kwa ajili ya mradi huo wa kutengeneza madawati.
Akipokea msaada huo, Mkuu wa mkoa wa Arusha Daudi Felex Ntibenda amelipongeza shirika hilo kwa msaada huo wa madawati na kuomba wananchi wengine na taasisi mbali mbali kusadia vifaa mbali mbali vya elimu.
Ntibenda, amezitaka taasisi zingine za ufundi na mikoa mingene kuja Arusha kujifunza teknolojia hiyo ya kutengeneza madawati na meza kwa kutumia mabaki ya chupa tupu  za maji na mifuko ya plastiki.
Mkuu huyo wa mkoa amesema kuwa teknolojia hiyo itasaidia sana kupunguza uchafuzi wa mazingira pamoja na kuongeza hajira kwa vijana wanao kusanya chupa tupu  na kuuza kwa taasisi hiyo

No comments:

Post a Comment