NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
WAAMUZI wa mchezo wa soka
mkoani Pwani wametakiwa kuhakikisha wanachezesha kwa kuzingatia sheria
17 za mchezo huo na kutoa maamuzi yaliyo sahihi ili wasiwe ni moja ya
chanzo cha susababisha migogoro n akuvunjika kwa baadhi ya michezo
wanayokuwa wakichezesha.
Kauli hiyo imetolewa na
Mwenyekiti wa Chama Cha Soka mkoani Pwani (COREFA) Hassan Hassanoo
wakati alipokuwa akifungua mafunzo kwa waamuzi wa mchezo wa soka wa
mkoa huo ambayo yaliyofanyika kwenye uwanja wa Shirika la Elimu Kibaha
Tumbi.
Hassano alisema kwamba mwamuzi
wa mchezo wa mpira ni sawa na na hakimu ambaye anapaswa kutoa maamuzi
yake kuzingatia sheria kanuni pamoja na taratibu zote ambazo zimewekwa
katika kuongoza mchezo wa soka ii kuweza kutimiza malengo ya kuweza
kuuendeleza zaidi kuanzia ngazi za chini hadi za juu.
“Mimi kikubwa ninachowaomba
waamuzi katika Mkoa wa Pwani tuwe makini sana katika kutimiza majukumu
yenu, kwani wakati mwingine michezo imekuwa ikivunjika na wengine kutoa
malalamikoi, kwa hiyo katika hili hakikisheni mnasimamia sheria zote 17
za mchezo huu wa soka katika Mkoa wetu wa Pwani na sio
vinginevyo,”alisema Hassanoo.
Aidha aliongeza kuwa suala la
kuwa mwamuzi wa mchezo wa soko ni wito na si suala la biashara kama
baadhi yao wanavyofanya kama sehemu ya kujiongezea kipato kwani mwamuzi
anapaswa kuhakikisha mchezo unakwisha salama na hata kama unavunjika
sababu iwe ambayo ni nje ya uwezo lakini siyo kusababishwa na mwamuzi.
“Kwa hiyo waamuzi mnapaswa
kujifunza kila mara kwa sababu sheria za soka hubadilika kila mara
ambapo kwa sasa zimekuwa zikibadilika kama fasheni kwa lengo la kuongeza
ladha ya mchezo wa soka hivyo lazima muendane na mabadiliko ya sheria
hizo ili kupunguza lawama ambazo zimekuwa zikitolewa ,” alisema
Hassanoo.
Aliwataka waamuzi wasibweteke
na madaraja waliyopo bali waongeze bidii ili wafike madaraja ya juu na
kuweza kuchezesha ligi kuu kama walivyo baadhi yao na waweze kufikia
kuchezesha michezo inayoandaliwa na Mashirikisho ya Soka Afrika CAF na
Dunia FIFA na mkoa utaendelea kutoa mafunzo mbalimbali.
Kwa upande wake mmoja ya
waamuzi ambaye alisoma risala ya waamuzi hao Kasule ambogo alisema kuwa
wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutolipwa posho
zao kwa wakati ambapo zamani walikuwa wakilipwa hata kabla ya mchezo.
Ambogo alisema kuwa pia
changamoto nyingine ni kukosa mafunzo hayo ya kujikumbusha sheria za
soka kwa muda mrefu hivyo kusababisha waamuzi kushindwa kupanda
madaraja kwa wakati na kuksa hata sifa za kuweza kuchezesha katika ligi
kuu ya Tanzania bara.
KOZI hiyo ambayo ilifanyika kwa
siku mbili kwa kuwashirikisha waamuzi wapatao 60 kutoka maeneo mbali
mbali ya Wilaya zilizopo katika Mkoa wa Pwani.
|
July 25, 2016
HASSANOO AWATAKA WAAMUZI WA MCHEZO WA SOKA WAZINGATIE SHERIA 17 NA KUACHANA NA TAMAA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment