Ibada
ya Mazishi ya aliekuwa Mkuu wa Vipindi na Afisa Mahusiano katika kituo
cha runinga cha Barmedas Tv cha Jijini Mwanza, Mwalimu Charles Sokoro,
imefanyika jana katika Kanisa la AICT Makongoro na kufuatiwa na mazishi
yaliyofanyika katika Makaburi ya Kitangiri.
Mwalimu
Sokoro ambae pia alikuwa mwalimu wa muziki wa Injili na Mwenyekiti wa
Kwaya ya AICT Makongoro, alifariki jumamosi Julai 16,2016 majira ya saa
mbili usiku katika Hospitali ya Rufaa Bugando baada ya kuugua kwa miezi
kadhaa.
Alizaliwa
mwaka julai mosi mwaka 1965 katika Kijiji cha Kahunda Wilaya ya
Sengerema mkoani Mwanza na hadi mauti yanamkuta alikuwa na umri wa 51
ambapo ameacha watoto wanne, alikuwa mgane.
|
Mchungaji Mika Ngusa kutoka TCRA akihubiri katika ibada ya mazishi ya marehemu Sokoro. |
Mkurugenzi wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari Tanzania, Abubakar Karsan, akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya Wanahabari |
Mkurugenzi wa Barmedas Tv, alikokuwa akifanya kazi Mwl.Sokoro |
Viongozi mbalimbali wa dini mkoani Mwanza, pamoja na waombolezaji wakiwa katika ibada ya marehemu Sokoro. |
Haleluya Benjamin kutoka Mtandao wa Wanahabari Watoto mkoani Mwanza pamoja na waombolezaji wengine wakiuaga mwili wa marehemu Sokoro |
Meneja wa Metro Fm ya Jijini Mwanza, na mwanachama wa BMG Tanzania, Alphonce Tonny Kapela, pamoja na waombolezaji wengine wakitoa wakiuaga mwili wa marehemu Sokoro |
Baadhi ya wafanyakazi wa Barmedas Tv pamoja na waombolezaji wengine wakiwa katika mazishi ya mwalimu Sokoro |
Mmoja wa watoto wa marehemu Sokoro (mwenye shati jeupe) akiwa na waombolezaji wengine katika mazishi ya Mwalimu Sokoro |
Shangazi wa marehemu akimwaga udongo ishara ya kuuaga mwili wa marehemu Sokoro |
aMkurugenzi wa Barmeds Tv akimwaga udongo ishara ya kuuaga mwili wa marehemu Sokoro |
Baadhi ya Waandishi wa Habari wa kundi la Whatsupp la BMG Tanzania, wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Barmedas Tv |
No comments:
Post a Comment