Waziri
wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe amesema Mahakama Kuu chini
ya kitengo kinachosimamia kesi za kuhujumu uchumi imetoa adhabu ya
kifungo na kulipa faini ya Sh29 bilioni kwa watu 12 baada ya kutiwa
hatiani.
Pia,
alisema Mahakama ya Mafisadi iliyoahidiwa na Rais John Magufuli wakati
wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana, itakapoanza itashugulikia kesi za
ufisadi zenye ushahidi.
Dk
Mwakyembe alisema hayo jana kwenye mahojiano katika kipindi cha 360
kinachorushwa moja kwa moja, asubuhi siku za wiki na Televisheni ya
Clouds.
“Tuna
kesi 176 za kuhujumu uchumi tangu Juni mwaka jana hadi sasa. Kesi 13
zimekamilika, watu 12 wamehukumiwa vifungo vya jela na tunawadai Sh29
bilioni kwa hiyo kama mtu alikuwa na ‘kastore’ tutauza tupate hiyo
pesa,” alisema Dk Mwakyembe.
Aliongeza: “Nchi ilipofikia tunataka tuachane na hizi tabia za udokozi unapopewa mamlaka ya kuhudumia umma.”
Alipoulizwa kuhusu mahakama ya mafisadi alisema: “Hatujaanzisha Mahakama, tumeanzisha divisheni (kitengo) ambacho kitasimamia kesi hizo kwa haraka na kwa weledi zaidi.”
Itakumbukwa
kuwa Aprili Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowasilisha hotuba
ya makadirio na matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu bungeni alisema
Serikali imeanzisha Divisheni ya Rushwa na Ufisadi ya Mahakama Kuu.
Majaliwa
alisema mahakama hiyo itaanza kushughulikia kesi 10. Dk Mwakyembe
alipoulizwa kama kuna kesi zozote zinazohusu EPA, Escrow au Richmond
zitakazo sikilizwa, alijibu: “Sheria tunayotumia ni kwamba, kesi za
jinai hazina vizuizi kwa upande wa Jamhuri.Hata kama ulichukuwa miaka 20
iliyopita, kama ushahidi unapatikana tutaendelea. Lakini hatuna
interest kufufua makaburi ya huko nyuma.”
Kuhusu mchakato wa Katiba inayopendekezwa alisema: “Ni kiporo ambacho tumepokea Serikali ya awamu ya tano na lazima tukimalize.”
Alisema kinachofanyika sasa ni kufuata Katiba kwa sababu mchakato huo ulisimama kupisha Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.
“Tusingeweza
kusimamisha uchaguzi kwa ajili ya kupiga kura ya maoni. Kwa hiyo
tunasubiri wenzetu NEC (Tume ya Taifa ya Uchaguzi) wawe tayari ili
mchakato uweze kuendelea,” alisema.
|
July 22, 2016
KESI ZA UHUJUMU UCHUMI ZAINGIZA BILIONI 29
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment