Mwenyekiti
mstaafu wa chama cha mapinduzi (CCM)dk.Jakaya Kikwete akipewa zawadi na
baadhi ya wazee wa wilayani Bagamoyo, kwenye sherehe za kumpokea na
kumkaribisha nyumbani baada ya kumaliza muda wake wa uongozi wa
chama,sherehe zilizofanyika juzi ukumbi wa chuo cha sanaa (TASUBA).
(Picha na Mwamvua Mwinyi)
……………………………………………………………………………….
Na Mwamvua Mwinyi,Bagamoyo- 26,July
MWENYEKITI
mstaafu wa chama cha mapinduzi (CCM),dk Jakaya Kikwete amesema ni ndoto
vyama vya upinzani kushinda katika chaguzi kuu zijazo kutokana na chama
tawala kuwa imara na kujidhatiti katika kutekeleza ilani yake na
kuwatumikia wananchi.
Aidha amesema anaimani nchi itaendelea kuwa na maendeleo makubwa na kuinua uchumi kutokana na kasi aliyonayo rais John Magufuli.
Sambamba na hayo dk.Kikwete
ameeleza kuwa kwasasa anahitaji kupumzika na atakuwa anajishughulisha
kilimo na ufugaji ambapo hayupo tayari kutoa ushauri wa mambo ya
kiserikali na chama kwani kazi hiyo ina wenyewe na wanatosha.
Dk Kikwete alisema anashukuru
mungu kipindi chake ameongoza na kuiacha nchi ikiwa na utulivu mkubwa
licha ya uchaguzi mkuu uliopita kupitia kwenye kipindi kigumu.
Aliyasema
hayo jana majira ya jioni huko mjini Bagamoyo kwenye ukumbi wa chuo cha
sanaa (TASUBA)wakati wa sherehe za kumkaribisha baada ya kustaafu na
kumkabidhi nafasi ya uenyekiti dk.John Magufuli.
“Namshukuru mungu nchi iko salama
na chama kiko imara nami kwa sasa nataka nipumzike sitajihusisha na
masuala ya kisiasa ama kiserikali nataka nipumzike badala yake
nitajikita katika shughuli za kijamii ikiwemo kufuga na kilimo”
“Mkija kufuata ushauri pale
mtakapohitaji ,lakini naomba mkija mje kwa ajili ya suala la maendeleo
nitakuwa tayari na sio kwa suala la kutoa ushauri kuhusu serikali hapana
kwani kwa sasa kuna viongozi ambao wanauwezo na nawaamini kwa kiasi
kikubwa”alisema Kikwete.
Dk
Kikwete hakuna kitu kilichokuwa kikimpa wakati mgumu kama chama ama
serikali kushindwa kufanikiwa malengo yake kwenye uongozi wake.
Alisema
hali ya kushindwa ilikuwa ikimpa wakati mgumu na kujiona endapo
angeshindwa basi angewaangusha Wanabagamoyo na Pwani nzima.
Dk.Kikwete alieleza kwamba
anamshukuru mungu katika uongozi wake aliweza kufanya kazi na kuleta
maendeleo makubwa na kuiacha nchi mahali pazuri na salama huku ikiwa
imetulia.
Aliwataka watanzania kumuombea na kumuunga mkono rais dk. John Magufuli ili aweze kuleta maendeleo .
Awali
wabunge wa mkoa huo wakiongozwa na mbunge wa jimbo la Bagamoyo dk
Shukuru Kawambwa alisema wataendelea kumuenzi Kikwete kwa kujenga mnara
wa kumbukumbu kwenye ofisi ya CCM mkoani Pwani
No comments:
Post a Comment