KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

July 24, 2016

KITUO CHA ALBINO BUHANGIJA SHINYANGA CHAWEKEWA TAA ZA SOLAR


Mafundi umeme kutoka kampuni ya wakandarasi wa umeme CSI Electrical Limited wanaojihusisha na kufunga umeme majumbani wakiendelea na zoezi la kufunga mitambo ya umeme wa solar katika kituo cha watoto wenye ulemavu wa ngozi (albino),wasiosikia na wasioona cha Buhangija katika manispaa ya Shinyanga.
Mafundi umeme wakiendelea kufunga moja ya mitambo ya umeme unaotumia nguvu ya jua katika kituo cha Buhangija...Kila mtambo una Panel 2 na jumla ya Panel zilizofungwa katika kituo hicho ni panel 13,thamani ya mradi wote ikiwa ni shilingi milioni 75.88 
Mgeni rasmi katika uzinduzi wa mradi wa Umeme wa Solar katika kituo cha Buhangija,Josephine Matiro akiwasili katika kituo hicho na kupokelewa na watoto wanaoishi katika kituo hicho
Mwakilishi wa Kampuni ya wakandarasi wa umeme -CSI Electrical Limited Joan Kahwa(katikakti) akimuonesha mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro (kulia) akimuonesha moja ya mitambo ya umeme wa jua katika kituo cha Buhangija.Kushoto ni Miss Tanzania 2012 Brigitte Alfred aliyefanikisha kuwepo kwa mradi huo 
CHANZO:MALUNDE BLOG

No comments:

Post a Comment