WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amesema Bara la Afrika bado linakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa
maji safi na salama hasa vijijini kwa sababu nchi zake bado hazijamudu
kuunganisha huduma hiyo katika maeneo hayo.
Kufuatia hali hiyo, Waziri Mkuu
amewataka wataalamu wa masuala ya maji watafute njia sahihi
itakayowezesha kutatua tatizo hilo kwa kutumia vyanzo mbalimbali vya
maji vilivyoko.
Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo
jana (Jumatatu, Julai 18, 2016) katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa
cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam wakati akifungua mkutano wa 10
wa Baraza la Mawaziri wa Maji wa Afrika (AMCOW) ambao unaokwenda
sambamba na maadhimisho ya Wiki ya Maji Afrika.
“Tunategemea baada ya kumazika
kwa mkutano huu wataalamu wetu wataondoka na maazimio mazuri ya kumaliza
tatizo la maji katika Bara letu kwa kutumia mito na maziwa ili
kufikisha maji kwa wananchi,” alisema.
Akizungumzia kwa upande wa
Tanzania alisema, suala la maji limepewa kipaumbele hata katika bajeti
ya mwaka huu na kwamba Serikali itahakikisha maji yanapatikana katika
maeneo yote ili kutimiza sera yake ya kila mwananchi kupata maji umbali
usiozidi mita 400.
Kwa upande wake Rais Mstaafu wa
Kenya Mwai Kibaki ambaye ni Mjumbe Maalumu wa UNESCO kwa ajili ya
masuala ya maji Barani Afrika alisema maji ni muhimu kwa maendeleo ya
uchumi, hivyo wataalamu wanatakiwa kuhakikisha huduma hiyo inapatika
katika maeneo yote.
Mkutano huo wa siku tano
unahudhuriwa Mawaziri wa Maji kutoka nchi 45 za Afrika na unaongozwa na
Waziri wa Maji na Mazingira wa Senegal Amadou Mansour Faye ambaye ni
Rais wa AMCOW.
|
July 19, 2016
MAJALIWA: BARA LA AFRIKA BADO LINAKABILIWA NA CHANGAMOTO YA UPATIKANAJI WA MAJI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment