Mlinzi wa Kampuni ya Ulinzi ya Imara, Samwel Arcado (39) amejinyonga
ndani ya chumba chake kwa madai ya kugundulika kuwa na maambukizi ya
virusi vya Ukimwi (VVU).
Mlinzi huyo ambaye ni mkazi wa Mtaa wa Mji wa
Zamani, Manispaa ya Mpanda alikutwa amejinyonga kwa kutumia shati.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Damas Nyanda alisema jana kuwa
uchunguzi kuhusu tukio hilo unaendelea.
Mwenyekiti wa mtaa huo, Margaret John alisema tukio hilo lilitokea jana saa kumi na moja alfajiri
ndani ya chumba alichokuwa akiishi Arcado.
Alisema Samwel alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya mara kwa mara, hali iliyosababisha kwenda
hospitali kufanyiwa uchunguzi wa afya yake, ambako aligundulika kuwa na
VVU.
John alisema baada ya kupatiwa majibu hayo alichanganyikiwa, hali
iliyosababisha utendaji wake wa kazi kuzorota.
Alisema kutokana na
kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi, mwajiri wake alitaka kumrejesha
nyumbani kwao mjini Sumbawanga mkoani Rukwa.
Hata hivyo, taarifa zinadai
kuwa siku ya safari ilipofika, mmoja wa wafanyakazi wenzake alifika
kwenye nyumba aliyokuwa amepanga kwa lengo la kumwamsha ili ajiandae,
lakini alipomgongea mlango hakujibiwa hali iliyompa shaka na kuwaamsha
wapangaji wengine.
Mwenyekiti huyo alisema mfanyakazi huyo na
wapangaji wenzake, walitoa taarifa kwa uongozi wa serikali ya mtaa na
ulipofika uliamuru mlango uvujwe na kukuta amejinyonga. Alisema walitoa
taarifa polisi ambao walifika na kuchukua mwili.
|
July 20, 2016
MLINZI WA KAMPUNI YA ULINZI AJINYONGA BAADA YA KUGUNDULIKA ANA VIRUSI VYA UKIMWI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment