Rais Barrack Obama wa Marekani
amewasihi wamerakani wajizue dhidi ya hisia kali baada ya Mmarekani
Mweusi kuwapiga risasi na kuwaua maafisa watatu wa polisi katika
shambulizi la pili la kulipiza kisasi dhidi ya polisi wazungu wanaowaua
wamarekani weusi.
Obama aliyasema hayo katika hotuba ya moja kwa moja kupitia kwa runinga kutoka ikulu ya WhiteHouse muda mchache tu baada ya mtu mmoja mweusi kuua maafisa watatu wa polisi hukohuko Baton Rouge alikouawa mtu mweusi Alton Sterling pasi na hatia yeyote majuma mawili yaliyopita. Hasira imekuwa ikitokota miongoni mwa watu weusi baada ya mtindo wa kuuawa kwa wanaume weusi na polisi wazungu kuendelea kwa muda mrefu ilihali hakuna hatua inayochukuliwa dhidi yao. Gavin Long ambaye ni mwanajeshi wa zamani alikuwa amerekodi ujumbe katika mji wa Dallas siku chache baada ya polisi watano kuuawa mjini humo katika shambulizi lililotekelezwa kulipiza kisasi cha mauaji ya Sterling.
Sasa imebainika kuwa Long alikuwa ameweka video
kwenye mtandao akilalamika jinsi polisi wanavyowatendea waamerika weusi
ambapo alitoa wito kwa wanaume weusi kujitolea kuokoa jamii yao.
Long mwenye umri wa miaka 29 aliwahi kuhudumu kama mwanajeshi wa Marekani . Rais Obama ameshauri watu weusi dhidi ya kutekeleza mashambulizi dhidi ya Polisi akisema mauaji ya kulipiza kisasi sio suluhisho la tatizo sugu la ubaguzi wa rangi bali utachochea uhasama zaidi dhidi yao na polisoi wazungu. CHANZO:BBC |
July 18, 2016
MWEUSI AWAUA POLISI WATATU MAREKANI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment