Mwanamuziki
wa Kongo Koffi Olomide ambaye anajulikana kwa ngoma zake kali ana
utajiri wa dola za Kimarekani milioni 18 karibu Shiliongi bilioni 40 za
Kitanzania kwa mujibu wa utafiti wa mwaka huu . Majina halisi ya Koffi ambaye pia ni muasisi la Quartier Latin International orchestra ni Antoine Christophe Agbepa Mumba alizaliwa mwaka Julai 13, 1956, mjini Kisangani nchini Kongo. Akiwa kijana alipenda kuimba na kupiga kitaa.
Alipata
nafasi ya kwenda kusoma nchini Ufaransa,vyanzo vinasema kwamba ana
Shahada ya pili katika Hisabati,nyingine ni Shahada ya kwanza katika
Uchumi, Shahada zote hizo alizisomea nchini Ufaransa
Alirudi
Kongo miaka ya sabini na kujiunga na kundi la Viva la Musica chini ya
Marehemu Papa Wemba akiwa mtunzi na mwandishi wa nyimbo.
Koffi alianzisha kundi lake la Quartier Latin mwaka 1986 ana kufanikiwa kupata wapenzi wengi Afrika na Ulaya . Ana tuzo mbalimbali kama vile Mwanamuziki Bora wa Afrika, na nyingine za Kora .Chanzo Mtandao wa Net Worth |
July 25, 2016
PAMOJA NA KUTIMULIWA KENYA, KOFFI OLOMIDE ANA MILIKI BILIONI SH.40 ZA KITANZANIA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment