Baada
ya vifaa vyao vya ofisi zikiwamo kompyuta 25 kushikiliwa na polisi kwa
miezi 10, hatimaye jana Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC)
wamerejeshewa.
Oktoba
mwaka jana, polisi walikwenda katika tawi la ofisi ya LHRC Kawe, kisha
kuchukua kompyuta za mezani 24 na mpakato tatu huku wakiwashikilia
waangalizi 25 wa uchaguzi, kwa kile ilichodai kituo hicho kilikuwa
kinakusanya na kusambaza taarifa za matokeo ya urais yasiyo rasmi.
Mkurugenzi
wa kituo hicho, Dk Hellen Kijo-Bisimba alithibitishia kupata vifaa
hivyo vilivyokuwa vikishikiliwa na Polisi Kanda Maalumu ya Dar es
Salaam.
Dk Bisimba alisema wiki iliyopita waliwapigia simu polisi kuwaomba kurejeshewa vifaa hivyo, zikiwamo simu 25.
“Jana
(juzi) polisi walitupigia simu.Leo (jana) tumekwenda kuchukua mali zetu
na zote zipo kamili isipokuwa kuna kompyuta moja haifanyika kazi,” alisema.
Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo, Simon Sirro alipopigiwa simu yake ilipokewa na msaidizi wake na kudai yupo mkutanoni.
|
July 19, 2016
POLISI WARUDISHA VIFAA VYA KITUO CHA SHERIA NA HAKI ZA BINADAMU (LHRC) VILIVYOKUWA VINASHIKILIWA TANGU MWAKA JANA BAADA YA UCHAGUZI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment