KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

July 25, 2016

PSPTB YAENDESHA SEMINA KWA WAKURUGENZI NA WAKUU WA IDARA MUHIMBILI

ps1
Msimamizi wa Ushauri na Utafiti (PSPTB), Amos Kazinza akitoa mada LEO katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Kulia ni Mkuu wa Idara ya Ugavi, Pindani Nyalile akiwa kwenye semina hiyo. Semina hiyo imelenga kutoa mafunzo kwa watendaji wa MNH ili waweze kuzingatia taratibu na sheria za manunuzi. Wakurugenzi na wakuu wa idara wa MNH wametakiwa kutoa haki wakati wa kutoa zabuni. Pia, wameshauriwa kutonunua bidhaa zilizopo chini ya kiwango.
ps2
Baadhi ya wakurugenzi na wakuu wa idara wakiwa kwenye semina hiyo ya siku tatu iliyoanza LEO katika hospitali hiyo.
ps3
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru (kulia) akifuatilia mada katika semina hiyo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Fedha, Gerald Jeremia akiwa katika semina hiyo LEO. Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Wateja, Aminieli Aligaesha akisikiliza jambo kwenye semina hiyo.
ps4
Mwenyekiti wa Bodi ya Zabuni katika hospitali hiyo, Dk Faraja Chiwanga akifuatilia mada kwenye semina hiyo.
Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)

No comments:

Post a Comment