Serikali
iko mbioni kutoa hatimiliki zaidi ya 25,000 kwa wakazi wa kata za
Kimara na Saranga zilizopo jijini Dar es Salaam ikiwa ni hatua ya
kurasimisha makazi holela.
Hayo
yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mratibu wa Mradi wa urasimishaji
wa makazi holela Kata za Kimara na Saranga, Bi Grace Masatu wakati wa
zoezi la ukaguzi wa maeneo ya mradi.
“Zoezi
za la upimaji linaenda sanjari na utambuzi wa mipaka,ujazaji wa
madodoso, uchoraji wa ramani za upimaji na mipangomiji,” alisema Masatu.
Viwanja
zaidi ya 25,000 vinatarajiwa kupimwa katika kata za Kimara na Saranga
ambapo hadi leo ramani za upimaji 14 na ramani sita (6) za mipangomiji
zenye jumla ya viwanja1028 ziko tayari na zimeshawasilishwa Wizara ya
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa ajli ya kupitishwa, alisema
Masatu.
Aidha,
Masatu amesema kuwa malengo ya mradi huo ni kuongeza thamani ya makazi
kwa kutoa hatimiliki na kutambua mipaka ya wakazi wa maeneo husika.
Kwa
upande wake, Afisa Mipango miji Mkuu, Bi Anna Macha, alisema kuwa hadi
sasa maeneo yaliyopimwa katika kata ya Kimara ni mtaa wa Kilungule A
wote pamoja na viwanja 724 vya mtaa wa Kilungule B, ambavyo
vimechukuliwa mahesabu ya upimaji kwa ajili kuandaa ramani.
Ameongeza
kuwa umetengenezwa mfumo maalum ambao unachukua taarifa za madodoso
zinazojazwa wakati wa utambuzi wa mipaka ya wamiliki wa maeneo husika.
Mfumo huo utaunganishwa na mfumo wa Kamishna wa Ardhi (MOLIS)
utakaorahisisha kufahamu idadi ya viwanja vilivyopimwa na kumilikishwa.
Naye
Mjumbe wa Mtaa wa Kilungule B, Bwana Claud Misri Silayo ameonyesha
kuridhishwa na zoezi zima la utambuzi na upimaji wa maeneo.
“
Nimefurahishwa na zoezi la upimaji kwani nitamiliki ardhi kisheria,
kihalali na nitafaidika na ardhi ninayomiliki kwa sababu mwisho wa zoezi
hili nitapata hatimiliki ambayo itaniwezesha kupata mikopo kwenye
taasisi za fedha,”alisema Silayo.
Urasimishaji
ni mwendelezo wa utambuzi wa makazi holela katika jiji la Dar es Salaam
unaotekelezwa chini ya Sheria ya Ardhi Na. 4 pamoja na Sheria ya
Mipangomiji
No comments:
Post a Comment