Mkuu wa Kambi ya wakimbizi Nduta mkoani Kigoma Peter Buluku .
………………………………………………………………………………………………………………
Na Jacquiline Mrisho – Kigoma
Serikali ya Jamuhuri ya Muungano
wa Tanzania imewasaidia jumla ya wakimbizi 55,320 kutoka Burundi kwa
kuwapa makazi na kuhakikisha ulinzi wa maisha yao katika Kambi ya Nduta
iliyopo wilayani Kibondo, Mkoa wa Kigoma.
Takwimu hizo zimetolewa na Mkuu
wa Kambi hiyo, Peter Buluku wakati akizungumza na mwandishi wa habari
hii juu ya hali halisi ya maisha ya wakimbizi wanaoishi katika kambi
hiyo pamoja na misaada inayotolewa na Serikali pamoja na Mashirika
yasiyo ya kiserikali.
Buluku amesema kuwa wakimbizi hao
ni raia wa Burundi ambao wamekimbia nchini kwao kutokana na vurugu
zilizojitokeza mwezi Aprili mwaka 2015 ambazo zilisababisha raia hao
kukimbilia nchi za jirani ikiwemo Tanzania.
“Sisi kama Serikali tunasaidia
wakimbizi kwa kuwapa ardhi kwa ajili ya makazi, kuhakikisha ulinzi na
usalama kwa wakimbizi,kupokea, kusajili na kutunza kumbukumbu za
wakimbizi pamoja na kuunganisha familia za wakimbizi zilizopoteana
wakati wa machafuko nchini mwao”, alisema Buluku.
Alifafanua kuwa kazi ya kutoa
huduma za kijamii zikiwemo za Afya, Chakula, ujenzi wa nyumba,
masoko,vyuo vya ufundi na miundombinu, Maji, huduma za haki za watoto na
wazee wasiojiweza, elimu pamoja na huduma za kutoa misaada ya kisheria
zinafanywa na mashirika yasiyo ya kiserikali yaliyojitolea kuwasaidia
wakimbizi hao.
Buluku aliongeza kuwa hadi sasa
kuna jumla ya mashirika yasiyo ya kiserikali 17 yanayoshirikiana na
Serikali kuhudumia Kambi hiyo ambapo huduma zote zinaongozwa na Shirika
la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) hivyo, kazi kubwa ya Serikali ni
kusimamia na kuhakikisha mashirika yote yanatoa huduma zinazofaa kwa
wakimbizi hao.
Mkuu huyo wa Kambi ametaja
changamoto kubwa inayoikabili kambi hiyo kuwa ni upungufu wa rasilimali
fedha kwa mashirika ambayo hali hiyo husababisha baadhi ya shughuli za
kuiwezesha kambi hiyo kutofanikiwa.
|
July 15, 2016
SERIKALI YASAIDIA WAKIMBIZI 55,320,NDUTA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment