Mashindano
ya kucheza muziki ya vijana maarufu kama Dance 100% yanayoandaliwa
na kituo cha televisheni cha East
Africa(EATV) yanatarajiwa kuanza Julai 16 mwaka katika viwanja
mbalimbali jijini Da r es Salaam. Yakitangazwa wakati wa uzinduzi huo
jijini Dar es Salaam ambapo Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania
imetangaza kuendelea kudhamini mashindano hayo.
Akiongea
na waandishi wa habari,Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina
Nkurlu alisema kuwa kampuni yake imekuwa
ikidhamini mashindano hayo kwa kipindi cha miaka minne mfululizo na
katika msimu wa mwaka huu imejidhatiti kwa kuweza kuendeleza gurudumu la
tasnia hii.
Nkurlu alisema kuwa Vodacom imeendelea kudhamni shindano kwa kutambua kuwa muziki na michezo ni maeneo ambao yanaweza
kutoa ajira kwa vijana na kuweza kuwakwamua kimaisha.
Aliongeza
kuwa Vodacom inatambua kuwa jukumu la kukabiliana na tatizo la ajira
hapa nchini sio la serikali peke
yake bali pia ni la watu wote ikiwemo makampuni,taasisi za umma na za
binafsi na ndio maana siku zote imekuwa mstari wa mbele katika kuunga
mkono jitihada za kupambana na tatizo la ajira kupitia nyanja mbalimbali
ikiwemo michezo, burudani na huduma mbalimbali
zinazotolewa na kampuni hiyo.
“Vodacom
tunaamini kuwa vijana wanaweza kuleta mapinduzi makubwa katika sekta
mbalimbali iwapo watawezeshwa,hivyo
tunadhamini mashindano haya tukiamini kuwa vijana wenye vipaji
wanaoshiriki wataweza kujitangaza na kujulikana ambapo katika siku za
usoni ni rahisi kujiajiri kupitia katika sanaa”Alisema Nkurlu.
Aliwataka
vijana waamke hususani wasichana wasibaki nyuma na watumie fursa kama
hizi ili waweze kujikomboa kiuchumi
“Suala la ajira sio kufanya kazi ofisini tu bali kuna njia nyingi za
kujiajiri na kujipatia mapato mojawapo ikiwa ni kupitia michezo,muziki
na sanaa nyingine na Vodacom siku zote tutakuwa mstari wa mbele kuunga
mkono jitihada za vijana kujikwamua kiuchumi”Alisisitiza
Nkurlu.
Naye
Mratibu wa Shindano hilo kutoka kituo cha televisheni cha Afrika
Mashariki ‘Brendansia Kileo alisema kuwa
mashindano haya kwa msimu wa mwaka huu yanadhaminiwa na Vodacom
Tanzania na kampuni ya Coca-Cola kama kinywaji rasmi cha Dance 100%
2016. Mashindano haya yataanza kufanyika jijini Dar es Salaam katika
viwanja vya leaders club, mashindano yataanza na raundi
tatu za usaili tarehe 16,23 na 30 Julai (2016) na kufuatia hatua za
robo na nusu fainali na kasha Fainali. Aliyataka makundi ya dansi
kujitokeza kujiandikisha kushiriki,Pia alitoa wito kwa wakazi wa Dar es
Salaam kujitokeza kushuhudia michuano ya usaili
“LIVE’ bila kiingilio chochote.
“Huu
ni mwaka wa Tano (5) East Africa Televisheni tunaandaa mashindano haya
na mara ya nne (4) chini ya udhamini
wa Vodacom Tanzania na mwaka hadi mwaka mashindano haya yamekuwa
yakiongezeka kupata umaarufu na kuwavutia vijana wengi kila kona ya nchi
yetu ambao wamekuwa wakijitokeza kushiriki na washindi wakiwa vinara
wakutangaza Dansi katika nchi mbali mbali kama T-
Africa, The Chocolate, Wakali sisi na WD”Alisema Kileo
Alisema kuwa mashindano hayo yatakuwa yanafanyika wikiendi kwa muda wa miezi mitatu vilevile yatakuwa
yakionyeshwa
na kituo cha televisheni cha East Afrika kila Jumapili saa moja kamili
usiku na kundi litakaloibuka
na ushindi litajinyakulia kitita cha shilingi Milioni saba (7) na
mshindi wa pili atajinyakulia kitita cha shilingi milioni (2) na mshindi
wa tatu atapongezwa na shilingi milioni mmoja (1) tofauti na miaka ya
nyuma. |
July 15, 2016
SHINDANO LA DANCE%KURINDIMA MWEZI HUU CHINI YA VODACOM TANZANIA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment