Jeshi
la Polisi mkoa wa Mbeya limeendelea kufanya misako, operesheni na doria
zenye tija katika maeneo mbalimbali ili kudhibiti uhalifu na wahalifu
na limekuwa likishirikiana na wananchi na wadau wengine katika jitihada
hizo za kukabiliana na uhalifu na wahalifu. Hata hivyo kuna matukio
mawili ya mauaji yameripotiwa kutokea katika wilaya za Chunya na
Mbarali kama ifuatavyo.
Tukio la kwanza.
NEEMA
NELSON MBUNGA [25], mfanyabiashara ya mazao, mkazi wa Mengele –
Chimala, aliuawa kwa kukatwa mapanga kichwani na mikononi akiwa amelala
chumbani kwake.
Tukio
hilo lilitokea tarehe 19.07.2016 majira ya saa 02:00hrs katika kijiji
cha Mengele, kata ya Chimala, tarafa ya Ilongo wilaya ya Mbarali.
Watu wawili wanashikiliwa na Polisi kuhusiana na tukio hilo akiwemo
kaka wa marehemu ANYAMISYE NELSON [34], mkazi wa Mengele – Chimala
ambaye alikuwa amelala chumba cha pili katika nyumba hiyo ambayo
haikuvunjwa sehemu yoyote na mtuhumiwa wa pili aliyekamatwa ni FREDY
LUPONELO CHOTA [32], mkazi wa Chimala. Chanzo cha tukio hilo bado
kinachunguzwa. Begi dogo la marehemu limekutwa eneo la shule ya msingi
Mengele umbali wa mita takribani 300 kutoka eneo la tukio likiwa na
vitambulisho na nguo.
Tukio la pili.
Watu
wawili SHIJA MIGUDA [40] na mke wake KABULA KATABI [35], wakazi wa
kitongoji cha Mpembe waliuawa kwa kukatwa mapanga mwilini wakiwa
wamelala nyumbani kwao, baada ya mlango wa nyumba kuvunjwa.
Tukio
hilo limetokea tarehe 19.07.2016 saa 02:30hrs kitongoji cha Mpembe,
kijiji cha Mwiji, kata ya Lualaje, tarafa ya Kipembawe, wilaya ya
Chunya. Chanzo cha tukio hili ni imani potofu za kishirikina kufuatia
marehemu hao kutuhumiwa kuwa ni wachawi hapo kijijini. Watuhumiwa ambao
ni majirani na marehemu walikimbia baada ya tukio, ufuatiliaji
unaendelea.
WITO:
Kaimu
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi wa Polisi EMANUEL .G
.LUKULA anatoa wito kwa jamii hasa wahalifu kuacha tabia ya kuwa na
tamaa ya utajiri wa haraka kwa kujipatia kipato haraka kwa njia ya
mkato / haramu badala yake wajishughulishe kwa kufanya kazi halali na
kupata kipato halali. Aidha Kamanda LUKULA anatoa rai kwa yeyote mwenye
taarifa juu ya mtu / watu waliohusika katika matukio hayo azitoe katika
mamlaka husika ili wakamatwe na sheria ichukue mkondo wake vinginevyo
wajisalimishe mara moja. Pia anaendelea kutoa wito kwa jamii kuepukana
na tabia ya kusadiki imani potofu za kishirikina kwani zina madhara
makubwa kwa jamii ikiwemo kupoteza nguvu kazi ya Taifa.
[EMANUEL G. LUKULA – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
|
July 22, 2016
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment