Tanzania
imeshauriwa kuongeza vyanzo vipya vya mapato ya ndani kwa ajili ya
maendeleo na kuchukua hatua kali dhidi ya fedha haramu badala ya
kutegemea mikopo ya nje.
Akizungumza
jana jijini Dar es Salaam katika utambulisho wa ripoti kuhusu Maendeleo
ya Uchumi barani Afrika ya mwaka 2016 ya Shirika la Maendeleo ya
Biashara la Umoja wa Mataifa (UNCTAD), Claudia Roethlisberger alisema
mikopo siyo njia endelevu ya maendeleo.
Alisema
licha ya ripoti hiyo kuonyesha kuwa madeni ya nchi za Afrika
yanahimilika, lakini Serikali za nchi za bara hilo zinatakiwa kuchukua
hatua ya kuzuia ukuaji wa haraka kwa madeni ili yasiwe mgogoro kama
ilivyotokea miaka ya mwishoni mwa 1980 na 1990.
Akizungumzia
ripoti hiyo, mchumi kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB), Prosper
Charle alisema mikopo yenye masharti nafuu ambayo Tanzania imekuwa
ikitegemea imepungua na kubaki yenye masharti magumu, hivyo inapaswa
kutafuta njia mbadala.
“Deni la Taifa kwa sasa linahimilika kwa sababu Tanzania ilikuwa ikipata mikopo yenye masharti nafuu ,” alisema.
Steven
Mwombela kutoka Taasisi ya Utafiti wa Sera za kuondoa Umasikini
(Repoa), alisema suluhisho kwa Tanzania ni kuwekeza kwenye ushirikiano
wa sekta ya umma na binafsi ili kupata maendeleo endelevu.
|
July 22, 2016
TANZANIA YATAHADHARISHWA KUONGEZEKA DENI LA TAIFA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment