Mwenyekiti wa CCM na Rais
Mstaafu, Dkt Jakaya Kikwete akiimba wimbo maalum kabla ya kufungua
Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) kwenye ukumbi wa
Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM mjini Dodoma leo Julai 22, 2016. Kushoto
ni Mwenyekiti wa CCM Mtarajiwa, Rais John Magufuli, Wapili kushoto ni
Makamu Mwenyekiti wa CCM , Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, kuliani ni
Makamu Mwenyekiti wa CCM , Bara, Philip Mangula na wapili kulia ni
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana. Mkutano huo ni kwa ajili ya
kupitisha jina la Rais Dk. John Pombe Magufuli kuwa mwenyekiti mpya wa
CCM ambapo kesho atathibitishwa na Mkutano Mkuu Maalum kwenye ukumbi wa
Dodoma Convention Centre mjini Dodoma
Dk. Jakaya Kikwete akizungumza na
wajumbe hao wakati akifungua mkutano huo amesema kikao hicho kilikuwa
ni cha mwisho kwake kama mwenyekiti wa CCM , Akawashukuru wajumbe hao
kwa kumpa ushirikiano kwa miaka kumi yote akiwa Mwenyekiti na akaongeza
kwamba kama Chama cha Mapinduzi hakikupasuka mwaka jana hakiwezi
kupasuka tena kitaendelea kudumu na kudumu zaidi.
Amesema Kulikuwa na mafisi
yaliyokuwa yakingojea mkono udondoke tu ili yaweze kudaka na kula lakini
yaliambulia patupu chama kilisimama kidete na kuendelea na mipango
mizuri kwa ajili ya watanzania.
(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DODOMA)
|
No comments:
Post a Comment