UBALOZI WA KUWAIT NCHINI WAKIPIGA JEKI CHUO CHA DIPLOMASIA
Balozi
wa Kuwait nchini, Mhe. Jasem Al-Najem akimkabidhi vitendea kazi
zikiwemo Kompyuta kwa Kaimu Mkuu wa Chuo cha Diplomasia (CFR), Dkt.
Bernard Achiula. Makabidhiano hayo yamefanyika leo katika Ofisi za Chuo
hicho zilizopo eneo la Kurasini Jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Mhe. Balozi Ramadhani Muombwa Mwinyi(wa kwanza kushoto) na
Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati, Mhe. Balozi Abdallah Kilima
wakiwa pamoja na Mhe. Jasem Al-Najem na Dkt. Achiula ambao
waliiwakilisha Wizara katika makabidhiano hayo.
Balozi
Mwinyi akiongea na Mhe. Jasem Al-Najem ambapo katika mazungumzo yao
walizungumzia namna ya kuimarisha uhusiano uliodumu kwa muada mrefu
baina ya mataifa ya Tanzania na Kuwait na alimshukuru kwa kukisaidia
chuo hicho ambacho kipo chini ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki na kumwomba kupanua wigo katika sekta ya Elimu
ikiwemo kuwa na program za mafunzo na kubadilishana uzoefu baina y anchi
hizi mbili.
No comments:
Post a Comment