Waziri wa afya,Maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Ummy Mwalimu akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ujenzi ya wodi ya wazazi kwenye kituo cha afya Gairo. |
Waziri Ummy Mwalimu akiwasikiliza watumishi wa kituo hicho cha afya(hawapo pichani),kushoto ni mbunge wa jimbo la Gairo Mhe.Ahmed Shabiby(wa kwanza kushoto)Mkuu wa Wilaya hiyo mhe.Siriel Mchembe(wa pili kulia) na wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa halmashauri bi.Agnes Mkandya |
Waziri Ummy akimsikiliza mwananchi(hayupo pichani)kwenye kituo cha afya gairo mara baada ya kuzindua ujenzi wa wodi ya wazazi,kulia ni bi. Agnes Mkandya Mkurugenzi wa halmashauri hiyo |
Waziri
wa afya akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa halmashauri
hiyo,mara baada ya kuzindua ujenzi wa wodi ya wazazi inayojengwa kwenye
kituo cha afya gairo.
(picha na wizara ya afya)
……………………………………………………………………………………….
Na.Catherine Sungura,Gairo
Halmashauri ya Wilaya ya Gairo wametakiwa kuweka kwenye mipango yake na kiwe kipaumbele chao ujenzi wa Hospitali ya wilaya.
Hayo yamesemwa na Waziri wa
Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati
akizindua ujenzi wa wodi ya wazazi inayojengwa kwenye kituo cha Afya
mjini hapa inayodhaminiwa na mbunge Ahmed Shabiby.
Waziri Ummy amesema wodi hiyo
ikikamilika itawasaidia akina mama wengi wa halmashauri Hiyo pamoja na
vijiji vya jirani kufika kituoni hapo kujifungua”suala ya uzazi kwa
mwanamke ni haki yake ya msingi,hivyo kuwa na wodi yao ni haki yao pia
na kwa afya zao na za watoto wanaojifungua”
Aidha,amesisitiza juu ya
utekelezwaji wa sera ya afya inayohusu matibabu bure kwa akina mama
wajawazito,wazee na watoto chini ya miaka mitano.
“Nazikumbusha hospitali na vituo
vya afya nchini kuwapa kipaumbele kwa kuwapatia matibabu makundi
haya,pia muweke dirisha litakaowahudumia wazee,na hii ndio muhimu
mlitekeleze”
Kwa upande wa watumishi,Waziri
Ummy Karnataka waendelee kufanya kazi kwa uadilifu kwa mujibu wa sheria
na taratibu Za taaluma zap na kuzingatia viapo vyao katika kuwahudumia
wananchi ili kusiwepo na malalamiko yatakayoleta matatizo.miongoni mwao.
“Nakuagiza Mkurugenzi wa
halmashauri uhakikishe unatatua changamoto za watumishi ikiwemo
kuwalipa posho za sare za kazi, likizo na stahiki zao nyingine
watumishi hawa”
Awali akisoma taarifa ya
Wilaya,mkuu wa wilaya hiyo bi. Siriel Mchembe alitaja changamoto kubwa
kwa upande wa huduma za afya ni kukosekana kwa hospitali ya Wilaya Mkuu
wa wilaya ya Gairo juu ya hali ya huduma za afya wilayani humo, alieleza
changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya afya ikiwemo ukosefu wa
hospitali ya wilaya, gari la kubebea wagonjwa, upungufu wa watumishi
pamoja na kutokuwepo kwa zahanati na vituo vya afya katika kata na
vijiji hali inayopelekea wananchi kuzifuata huduma za afya umbali mrefu.
|
No comments:
Post a Comment