Wafanyakazi
wa benki ya CRDB tawi la Mlimani City wakiwa katika picha ya pamoja
mara baada ya kufika katika ufukwe wa Milenium Bagamoyo Mkoani Pwani
mwishoni wa wiki, Wafanyakazi hao ikiwa ni utamaduni wao wa kila mwaka
kutembelea sehemu mbalimbali kwaajili ya kufurahi pamoja, kujenga
mahusiano mazuri wakati wa kazi pamoja na kunywa na kula pamoja.
Akizungumza
na Globu ya Jamii, Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Mlimani City, Allen
Killango amesema kuwa wameamua kupumzika pamoja, kula na kunjwa pamoja
mwishoni mwa wiki kwaajili ya kujenga mahusiano mazuri wakati wa kazi
ikiwa ni siku mhimu sana kwao ambayo hufanyika kila mwaka.
Katika
Mapumziko hayo ya wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Mlimani City
walikuwa na michezo mbalimbali ambayo walishiriki kama Mpira wa Mikuu
kwa wote, Kuvuta Kamba, kukimbia na ndimu kwenye vijiko, Mpira wa
wavu(Voleball) na kukimbia na Magunia.
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Mlimani City wakiwasili katika ufukwe wa Mileniam Bagamoyo Mkoani Pwani.
No comments:
Post a Comment