WAZIRI
Mkuu, Kassim Majaliwa amepiga marufuku matumizi ya viberiti, mishumaa
na hita za kuchemshia maji kwa wanafunzi wa bweni ili kuepusha majanga
ya moto na atakayekutwa, atachukuliwa hatua kali.
“Kuna
tabia ya baadhi ya wanafunzi hasa wa masomo ya fizikia kutengeneza
vifaa vya kienyeji vya kuchemsha maji mabwenini, jambo hili ni la hatari
kwani linaweza kusababisha ajali ya moto, hivyo ni marukufu kwa
mwanafunzi kutumia vifaa hivyo,” alisema.
Waziri
Mkuu alitoa agizo hilo jana katika harambee ya kuchangisha fedha za
ujenzi wa majengo ya Shule ya Sekondari Lindi, yaliyoungua moto usiku wa
kuamkia Julai 10, mwaka huu.
Katika
ajali hiyo shule imeathirika kwa asilimia 34 baada ya vyumba tisa vya
madarasa, jengo lenye matundu 26 ya vyoo na jengo la maabara ya kemia na
fizikia yameungua na kusababishia hasara ya Sh milioni 682.78.
Waziri
Mkuu alisema kwa namna ambavyo majengo hayo yameungua, ni vema
yakavunjwa na kujengwa upya. Aliwataka kutumia nafasi hiyo kujenga jengo
la ghorofa ili kutumia eneo dogo kwa kujenga madarasa mengi.
Pia
alimuagiza Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi kuhakikisha fedha
zitakazopatikana katika harambee hiyo, zinatumika kama ilivyokusudiwa.
Harambee
ilihudhuriwa na mke wa Waziri Mkuu, Mary Majaliwa, mke wa Rais mstaafu
wa Awamu ya Nne, Mama Salma Kikwete, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima
Dendego na wadau wa maendeleo na wanafunzi waliosoma shule hiyo akiwemo
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Ramo Makani.
Katika
hatua nyingine, Waziri Mkuu amezitaka taasisi mbalimbali nchini kufunga
vifaa vya kuzimia moto katika majengo yao kwa ajili ya kuvitumia pindi
ajali za moto zinapotokea.
|
July 18, 2016
WAZIRI MKUU APIGA MARUFUKU WANAFUNZI KUTUMIA MISHUMAA VIBERITI MABWENINI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment