Mkuu wa wilaya ya Arusha,Gabriel Daqarro
……………………………………………………………
Na Mahmoud Ahmad Arusha,
Hatimaye halmashauri
ya jiji la Arusha imetekeleza agizo lililotolewa na mkuu wa mkoa
wa Arusha,Mrisho Gambo la kulipa madeni yote ya walimu wa shule za
msingi na sekondari jijini Arusha ambapo jumla ya sh,
169 milioni zimelipwa kwa ajili ya walimu hao.
Fedha hizo ni zile ambazo zilikuwa ni madeni ya walimu waliyokuwa wakidai kwa muda mrefu katika Jiji la Arusha zimelipwa ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Mkuu wa Mkoa wa Arusha alilolitoa hivi karibuni.

Gambo, alipokutana na walimu wa shule za
msingi na sekondari Mkoani Arusha alipokea malalamiko mengi
moja ya malalamiko ni madai sugu ya walimu na
ndipo alipoiagiza halmashauri zote na jiji Mkoani Arusha
kulipa madeni hayo ndani ya siku 14.
Katika kutekeleza maagizo hayo,Mkuu wa wilaya ya
Arusha,Gabriel Daqarro alisema Jiji limetekeleza ndani ya siku mbili na
kufanikiwa kulipa kiasi hicho cha fedha kwa walimu wote wa msingi na
sekondari.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari jijini hapa Daqarro alisema Jiji la Arusha lina jumla ya walimu 701wa msingi na sekondari na madai hayo yalikuwa ya kipindi cha mwaka 2015/16 ambapo walikuwa wakidai kiasi cha sh,16 milioni na Sasa wamelipwa fedha zote na kwamba hakuna madai yoyote.
Alisema serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais John Magufuli inawajali na kuwalinda walimu wote na kuwapa stahili zao za msingi kwa wakati bila ya kipingamizi chochote.
Mkuu huyo alisema walimu walikuwa wakidai stahilizao za muda mrefu ikiwa ni pamoja na fedha za kujikimu,likizo,nauli,matibabu na upandishwaji madaraka na fedhahizo zote wamelipwa.
Alisema kwa sasa serikali ya wilaya ya Arusha inataka kuona walimu wakifanya majukumu yao ya msingi katika kupandisha elimu ikiwa ni pamoja na kufundisha wanafunzi bila ya kuwa na msongo wa mawazo.
Akizungumzia upatikanaji wa fedha hizo kwa muda huo mfupi alisema Halmashauri ya Jiji la Arusha iliamua kusitisha malipo yasiyokuwa ya lazima na kuondoa malipo ambayo yalikuwa kinyume na taratibu zikiwemo posho za madiwani na ndio maana fedha hizo zimepatikana.
Mkuu wa wilaya alisema sio kwamba fedha za kuwalipa walimu zilikuwa hazipo bali zilikuwa zikilipa vitu vilivyo nje ya utaratibu na kutokana na usimamizi wa Mkurugenzi wa Jiji la Arusha,Athumani Kihamia ameweza kubana mianya yote ya ulaji fedha hizo.
‘’Fedha nyingi za Jiji la Arusha zilikuwa zikilipwa kiholela holela na kufanya walimu kuteseka nakuumia pasipokuwa na sababu za msingi’’ Kwa sasa mianya hiyo imezibwa na ndio maana sasa fedha zinaonekana na zinalipa wahusika wenye kudai madeni yao ya muhimu kama haya ya walimu’’alisema Daqarro

Alisema kwamba wapinzani hususani Chadema wamekuwa wakitumia ma dai ya walimu nchini kama hoja ya msingi na sasa serikali imeamua kutekeleza madai hayo wanaanza kubeza.
Alisisitiza kwamba madiwani wa Chadema jijini Arusha waliamua kujiongezea posho kutoka sh,60,000 hadi 80,000 kinyume na utaratibu na kuhusu hoja kwamba walikuta posho hizo kabla ya kuingia madarakani haina mashiko.
“Hawa wamejiongezea posho kutoka sh,60,000 hadi 80,000 kinyume na utaratibu na wanasema kwamba wamezikuta hizi posho kwanini miezi minane waliyoingia wasizifute kama ziko kinyume?” alisema Daqarro
Hata hivyo,alisema kwamba ni jambo la ajabu kuona diwani wa kata ya Kaloleni iliyopo katikati ya mji akilipwa sh,80,000 kama posho ya nauli ilhali mtu akisafiri kutoka Dar es salaam hadi Arusha analipa nauli kiasi cha sh,30,0000.
Alisisitiza kwamba madiwani wa Chadema jijini Arusha waliamua kujiongezea posho kutoka sh,60,000 hadi 80,000 kinyume na utaratibu na kuhusu hoja kwamba walikuta posho hizo kabla ya kuingia madarakani haina mashiko.
“Hawa wamejiongezea posho kutoka sh,60,000 hadi 80,000 kinyume na utaratibu na wanasema kwamba wamezikuta hizi posho kwanini miezi minane waliyoingia wasizifute kama ziko kinyume?”
Hata hivyo,alisema kwamba ni jambo la ajabu kuona diwani wa kata ya Kaloleni iliyopo katikati ya mji akilipwa sh,80,000 kama posho ya nauli ilhali mtu akisafiri kutoka Dar es salaam hadi Arusha analipa nauli kiasi cha sh,30,0000.
No comments:
Post a Comment