Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk.
Hamisi Kigwangalla amefanya ziara ya kikazi katika Wilaya ya Mlele na
kutembelea Hospitali ya Mlele ya Wilaya hiyo pamoja na Hospitali ya
Mpanda iliyopo Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi huku akitoa maagizo
mbalimbali ya kiutendaji.
Katika
ziara yake katika Hospitali ya Mlele, Dk.Kigwangalla amewaagiza
viongozi wa Serikali wa Wilaya na ule wa Hospitali hiyo kuhakikisha
wanakamilisha mambo muhimu ikiwemo ujenzi wa chumba cha upasuaji, jengo
la kuhifadhia mahiti na vitu vingine huku akitaka ndani ya miezi mitatu
view vimekamilika.
Akiwa
katika Hospitali hiyo ya Mlele, Dk.Kigwangalla ameweza kutembelea
sehemu mbalimbali za hospitali pamoja na kukagua ujenzi wa majengo ya
Chumba cha upasuaji, chumba cha kuhifadhia maiti na majengo mengine
ambapo amemtaka Mkuu wa Wilaya kuhakikisha wanafanya juhudi
wanakamilisha kwa wakati majengo hayo ili wananchi wapate huduma bora.
Kwa
upande wa ziara yake hiyo katika Wilaya ya Tanganyika yaliyopo makao
makuu ya Mkoa wa Katavi, Dk. Kigwangalla ameweza kutembelea Hospitali ya
Mpanda ambayo kwa sasa inahudumia kama Hospitali ya Mkoa ambapo napo
ameagiza kufanyiwa marekebisho mbalimbali ikiwemo kuzingatia masuala
usafi.
Aidha,
ametoa maagizo kuhakikisha wanafunga mfumo wa malipo wa kisasa katika
vyanzo vyote vya mapato ili kukusanya pesa nyingi zaidi zitakazoweza
kuendesha huduma za Afya ndani ya Hospitali hiyo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na baadhi ya viongozi na watendaji wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mlele, Mkoani Katavi. |
Mkuu wa Wilaya ya Mlele, Bi.Rachel Kasanda akisoma taarifa kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla (katikati) |
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na watendaji wa Wilaya ya Mlele |
No comments:
Post a Comment