Kufuatia
mijadala iliyotokea katika mitandao ya kijamii wiki iliyopita
iliyolenga kutafsiri kudorola kwa uchumi wa nchi baada ya kupungua kwa
idadi ya mauzo katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) kwa asilimia
81, soko hilo limefafanua kuwa mauzo yake hayawiani na mwenendo wa
uchumi wa nchi.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Meneja Biashara na
Mauzo DSE, Patrick Mususa amefafanua kuwa kiashiria hicho hakikuwa
sahihi katika kutafsiri hali ya uchumi wa nchi.
Mususa
amesema sababu iliyopeleka idadi ya mauzo kushuka ni kutokana na
kupungua kwa uhitaji pamoja na kushuka kwa bei za hisa kwa wiki husika.
“Hakuna
uhusiano na uwiano baina ya idadi ya mauzo ya soko la hisa na uchumi wa
nchi, na mauzo ya soko hilo si kiashiria sahihi kutumiwa katika
kutafsiri mwenendo wa uchumi wa nchi,” amesema na kuongeza.
“Wiki
iliyopita punguzo la idadi ya mauzo ya hisa ilikuwa asilimia 81 ambapo
ilikuwa bilioni 1.7 idadi ilipungua kwa sababu wiki iliyopita ilikuwa
fupi yaani ilikuwa na siku nne za kazi, pia soko huwa linaendeshwa na
wanahisa wenyewe ambao huangalia mahitaji yao husika hivyo kushuka kwa
idadi ya mauzo kuna tegemea na bei husika ya hisa na mahitaji yake kwa
wiki hiyo,”
Aidha
Mususa amesema kuwa DSE haina kampuni za kutosha zinazowakilisha sekta
nyeti zinazoshikilia uchumi kutokana kwamba takribani kampuni 17 za
ndani ndizo zilizoorodheshwa.
“Hakuna
kampuni za kutosha ili kutafsiri uwiano wa uchumi wa nchi, mfano DSE
haina kampuni za simu ina maana sekta ya mawasiliano haijaorodheshwa,
kwa upande wa sekta ya viwanda kampuni za simenti, bia na sigara ndizo
zilizoorodheshwa pekee,”
Hata
hivyo, Mususa amesema kuna ongezeko la mauzo ya idadi ya hisa kwa wiki
iliyopita zaidi ya mara tisa na kufikia bilioni 16.4 kutoka bilioni 1.7.
“Ukubwa wa mtaji wa soko uneongezeka kwa asilimia 3.9 kutoka trilioni 20.8 hadi 21.6 trilioni.” amesema.
Mususa
amewataka wafanyabiashara wadogo, wa kati na wakubwa kuorodhesha
kampuni zao katika soko hilo ili kuongeza mitaji ya kampuni zao.
“Wafanyabiashara
na jamii kwa ujumla tunawashauri kushirikiana na DSE ili kupata fursa
ya kujitangaza, na kupata mitaji,” amesema
No comments:
Post a Comment