JARIDA
mashuhuri duniani la Forbes, limezitaja ndege aina ya Bombardier Dash8
Q400, ambazo tayari Tanzania imezinunua kuwa ni zenye usalama,
zinazotumia mafuta kidogo. Limetabiri kuwa zitakuwa nguzo muhimu kwa
usafiri wa bei nafuu kwa nchi mbalimbali.
Kwa
mujibu wa makala iliyochapishwa na jarida hilo ikiwa na kichwa cha
habari “Can Bombardier’s Q400 Save Regional Air Service in the US?”,
mwandishi anafafanua faida ya ndege hizo, ikilinganishwa na ndege
nyingine zinazofanya usafiri wa ndani nchini Marekani.
“Bombadier
ina kasi nzuri na ya kutosheleza mahitaji ya safari za ndani kwa
kiwango cha kuwa na faida zaidi kibiashara, ikilinganishwa na ndege
nyingine za aina yake kama ATR,” linaandika jarida hilo la Forbes.
Aidha,
jarida hilo linataja faida nyingine ya ndege hizo kuwa ni uwezo wa
kutumia mafuta kidogo, jambo litakalosaidia kupunguza gharama za usafiri
huo wa ndege nchini kwa wasafiri wa ndani. Jarida hilo linafafanua kuwa
kiwango kidogo cha mafuta, kinachotumiwa na ndege hizo, kunazifanya
kuwa na ufanisi wa asilimia kati ya 48 mpaka 50 zaidi ya ndege nyingine.
Forbes
linasisitiza kuwa kutokana na gharama za matengenezo kupanda na gharama
nyingine za uendeshaji, ikiwemo mishahara mizuri kwa marubani, kuna
uwezekano mkubwa kwa Bombardier kuendeshwa kwa bei rahisi na ikauza
tiketi kwa bei rahisi zaidi kuliko ndege nyingine.
“Kwa
sasa tunakadiria kuwa ndege aina ya Bombardier, ndizo zitakuwa mbadala
na zitashika njia nyingi za ndani (Marekani) kwa kiasi cha asilimia 50
hadi 60 na zitasaidia kurejesha usafiri uliositishwa kutokana na gharama
kubwa kwa ndege nyingine katika viwanja takribani 20,” linafafanua
jarida hilo.
No comments:
Post a Comment