Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akizungumza na viongozi wa makampuni mbalimbali kutoka Korea ya Kusini
ambao wamekuja Tanzania kuona fursa mbalimbali za uwekezaji. Mazungumzo
hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Septemba
27, 2016. Kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi ambaye pia ni Mbunge wa Ilemela, Angelina Mabula (Picha na Ofisi
ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa makampuni mbalimbali ya
Korea Kusini ambao wapo nchini kuona fursa mbalimbali za uwekezaji
nchini. Picha hiyo ilitanguliwa na mazungumzo yaliyofanyika Ofisini kwa
Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Septemba 27. Watatu kulia ni Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mbula. (Picha
na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu , Kassim Majaliwa
akikabidhiwa jezi yanye maneno Hapa Kazi Tu iliyotolewa na wawekezaji
kutoka Korea ya Kusini waliokuja nchini kuona fursa mbalimbali za
uwekezaji. Awali Waziri Mkuu alizungumza na wawekezaji hao ofisini
kwake jijini Dar es salaam Septemba 27, 2016. Kulia ni Naibu Waziri wa
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, ambaye pia ni Mbunge wa Ilemela,
Angelina Mabula. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
……………………………………………………………………
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amekutana na wawekezaji wa kampuni tisa za nchini Korea Kusini na
kumuahidi kushirikiana na Serikali ya Tanzania kuwekeza katika sekta ya
kilimo, viwanda, maji, miundombinu, elimu, afya na michezo.
Wawekezaji hao wanatoka kampuni
ya Sima textile, ESM, Jusung Solar Engineering, Seongnam City FC, Yeong
Yang City Korea,Ulsan Vocational Training, Egis Smart City, MBN
Akizungumza na wawekezaji hao
jana jioni (Jumanne, Septemba 27, 2016) kwa niaba ya Mhe. Rais Dk. John
Magufuli, Waziri Mkuu alisema kwamba Tanzania ni sehemu salama kwa
uwekezaji ikiwa na fursa za uwekezaji kwenye sekta nyingi kama
miundombinu, kilimo na viwanda. Licha ya mazingira mazuri ya uwekezaji
pia aliwahahakishia ulinzi kwenye uwekezaji wao
Waziri Mkuu alisema Korea ya
Kusini inashirikiana vizuri na Tanzania hivyo wanatarajia mengi kutoka
nchini huko kupitia wawekezaji hao.
Wawekezaji hao tayari wamefanya
mazungumzo na viongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela jijinii
Mwanza na kusaini Hati ya Makubaliano (MoU) kwa ajili ya miradi minne
ikiwemo ya ujenzi wa miundombinu ya maji, kiwanda cha nguo, zana kubwa
za kilimo na mafunzo ya ufundi.
Kwa upande wake Mkuu wa Msafara
huo, Bw. Son Young Soo alisema amefurahishwa na ziara waliyofanya nchini
na wapo tayari kuwekeza nchini.
Naye, Bw. Jihyun Kim wa kampuni
ya Yeong Yang City Korea ambayo inashughulikia masuala ya kilimo cha
mbogamboga alisema watawekeza kwenye kilimo hususan cha zao la pilipili
na watajenga kiwanda kwa ajili ya usindikaji.
Naye Mkurugenzi wa Klabu ya Soka
ya Seongnam Bw. Suk Hoon Lee alisema klabu yake ipo tayari kuwekeza
katika shule ya michezo kwa vijana ili kuongeza kasi ya maendeleo ya
soka.
No comments:
Post a Comment