Baada
ya Msajili wa Vyama vya Siasa kutangaza kuwa, Prof. Lipumba bado ni
mwenyekiti halali wa Chama cha Wananchi (CUF), jana kiongozi huyo
aliandamana na wananchi na wananchama wa CUF hadi Makao Makuu ya Chama
hicho yaliyopo Buguruni jijini Dar es Salaam.
Akiwa ndani ya ofisi za chama, Prof. Lipumba alipata wasaa wa kuzungumza na waandishi wa habari na alikuwa na haya yakueleza;
"Mimi
ni kweli niliandika barua ya kujiuzulu, tarehe 5 Agosti mwaka jana,
lakini baada ya uchaguzi wazee walikuja kuoniomba nirejee kwenye nafasi
ya uenyekiti kwa sababu hali ya chama haikuwa nzuri kitaifa, alisema
Prof. Lipumba
"Tarehe
8 nwezi wa 6 niliandika barua ya kutengua barua yangu ya kujiuzulu na
kwa mujibu wa katiba yetu (CUF) kujiuzulu kwako kutakuwa kamili endapo
mamlaka iliyokutua/kuchagua itaridhia maamuzi yako, hivyo Mkutano Mkuu
haukuwa umekutana kupitisha barua yangu ya kujiuzulu hivyo nilivyoandika
barua ya kutengua, nilirudi kuwa Mwenyekiti wa CUF.
"Baada
ya mvutano mrefu, tuliandika barua kwenda kwa Msajili wa Vyama,
akamuita Katibu Mkuu wa CUF na timu yake, akawaita na walalamikaji, na
wazee pamoja na mimi ili aweze kulisuluhisha.
"Na
baada ya yeye kusikiliza, ametoa msimamo wake kuhusu mgogoro wa uongozi
wa CUF ambapo amesema mimi bado ni mwenyekiti halali wa CUF hadi sasa",
alisema Prof. Lipumba
Katika
msimamo uliotolewa na msajili wa vyama akielezea kwanini Prof. Lipumba
ni mwenyekiti halali wa CUF alisema kuwa ni kwa sababu Mkutano Mkuu
haujaipitisha barua yake ya kujiuzulu wala haujakataa barua yake ya
kurejea kazini, lakini alichoambiwa ni kuwa asienze kazi Juni 10 kama
alivyokuwa ameeleza kwenye barua yake.
Aidha,
Prof. Lipumba alihitimisha kwa kusema kuwa Kamati iliyoteuliwa kuongoza
chama ni batili kwa sababu hata kikao kilichowateua ni batili na hivyo
kamati hiyo isijaribu kuongoza chama hicho kwani yeye ndiye mwenyekiti
wa CUF.
No comments:
Post a Comment