Viongozi wa serikali na Jeshi la polisi wakipata maelezo jinsi huduma zinavyotolewa katika Zahanati Mwendo
Viongozi wa serikali na Jeshi la polisi wakipata maelezo jinsi huduma zinavyotolewa katika Zahanati Mwendo
Madereva wakipima afya zao
Mwonekano wa Zahanati Mwendo kwa nje
……………………………………………………………….
-Wananchi wapata mafunzo ya unywaji kistaarabu
Huduma ya Zahanati Mwendo ambayo
imebuniwa na kampuni ya TBL Group katika maadhimisho ya Wiki ya Nenda
Kwa Usalama barabarani kwa ajili ya kupima afya za madereva imekuwa
kivutio kikubwa mkoani Geita ambako maadhimisho haya yamezinduliwa
kitaifa na idadi kubwa ya madereva na wananchi wanaendelea kujitokeza
kupima afya zao kwa wingi na kupatiwa matibabu na ushauri nasaha.
Madaktari maalumu waliopo kwenye
gari la kufanyia vipimo la Zahanati Mwendo muda wote tangia kuwasili
mkoani Geita wamekuwa na kazi kubwa ya kutoa huduma kwa madereva wengi
na wanaendelea kujitokeza kufanyiwa vipimo siku hadi siku.
Meneja Mawasiliano wa TBL Group
,Amanda Walter,amesema inavutia kuona watanzania wengi wanahitaji
huduma ya kupimwa afya na kumekuwepo na mwitikio mkubwa wa madereva na
wananchi wanaotembelea Zahanati Mwendo.
Alisema pia kuwa wananchi wengi
wamejitokeza katika semina ya Mafunzo ya Unywaji wa Kistaarabu
yaliyofanyika katika kituo Kikuu cha mabasi cha Geita ambapo walipata
fursa ya kujua madhara ya matumizi ya vinywaji vyenye kilevi kupindukia.
”Wiki ya Usalama ya mwaka huu
imekuwa na mwamko mkubwa hususani wananchi walivyojitokeza kwa wingi
katika mafunzo haya ya Unywaji wa Kistaarabu na mengine yanayohusina na
Usalama barabarani.TBL Group tunaendelea kushirikiana na serikali na
wadau wengine katika kampeni za Usalama kwa lengo la kupunguza matukio
ya ajali nchini”Alisema.
Rehema Nyoki,mkazi wa Geita
ambaye amehudhuria mafunzo ya Unywaji wa Kistaarabu akiongea kwa niaba
ya wenzake aliipongeza kampuni ya TBL Group kwa kuendesha semina za
uhamasishaji unywaji kistaarabu na alitoa ombi mafunzo hayo yafikishwe
sehemu mbalimbali nchini kwa kuwa ipo idadi ya waathirika wengi wa
kutumia vinywaji vyenye kilevi kupita kiasi kwenye jamii ambao
wanaishia kupata matatizo ya kila aina.
No comments:
Post a Comment