Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kesho anatarajiwa kuzindua ndege
mbili mpya aina ya Bombardier Q 400 zilizonunuliwa na Serikali hivi
karibuni.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi) Dkt. Leornard Chamuriho
amesema maandalizi yote kwa ajili ya uzinduzi wa ndege hizo yamekamilika
na uzinduzi huo utafanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere (JNIA) kuanzia saa mbili asubuhi.
“Tunawaomba wanahabari na
wananchi kujitokeza kwa wingi katika uzinduzi huo ili waone utekelezaji
wa ahadi wa Serikali katika mkakati wa kuhuisha usafiri wa Anga hapa
nchini”, amesema Dkt. Chamuriho.
Ndege hizo aina ya Bombardier Q
400 zenye uwezo wa kubeba abiria 76 kila moja zimetengenezwa nchini
Canada na zitahudumia soko la ndani ndani na nchi za jirani zitakapoanza
kazi.
No comments:
Post a Comment