KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

September 29, 2016

SERIKALI IMETOA BIL.2 KUJENGWA GATI NYAMISATI

kibi2
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
SERIKALI imeanza kutenga fedha sh. bil.2 ambazo tayari zimeshapelekwa wizara ya ujenzi ,ili kujengwa gati itakayohudumia wananchi wa Nyamisati wilayani Kibiti,Mafia na Rufiji.
Aidha serikali inafanya utaratibu wa kutafuta boti moja kubwa ambayo itaweza kuhimili nguvu ya maji na kukatisha katika maeno hayo.
Waziri mkuu Kassim Majaliwa aliyazungumza hayo kwenye mkutano wa hadhara wa wananchi huko Nyamisati wilaya ya Kibiti,mkoani Pwani.
Alisema serikali imedhamiria kuimarisha na kuondoa kero iliyopo kwasasa wanayopata wananchi baada ya gati la awali kubomoka kutokana na kushindwa kuhimili nguvu ya maji.
Alisema kipindi cha nyuma halmashauri yenyewe ilijenga gati hiyo kwa kiasi cha sh.mil.400 lakini ilibomoka kutokana na wingi wa maji .
“Wilaya ya mafia waliizungumzia vizuri sana kuwa ni tumaini lao,na mimi nilidhani watazungumzia kitu kipya lakini wameipenda sana Nyamisati,kwahiyo wakizungumza kitu ambacho nakifahamu,lakini serikali inajua gati hii inatumika na wilaya yote ya Mafia hivyo ni lazima tuimarishe”alisema Majaliwa.
Majaliwa alisema kwasasa watu wanapata shida ya kukwida nguo ndipo upande boti lakini anatarajia baada ya kujengwa gati hiyo kero hiyo itabaki historia.
Alieleza kuwa gati hiyo itajengwa na fedha imeshatengwa na kupelekwa wizara ya ujenzi waende kushughulikia kuijengajenga kwani barabara ni kubwa na gati ni tegemeo la wilaya yote ya Mafia.
Hata hivyo alisema mbinge wa jimbo la Kibiti,Ally Ung’ando ,amekuwa akisema mara kwa mara na kung’ang’ania juu ya suala hilo hivyo majibu yake ni hayo wananachi wawe na subira.
Alisema masuala ya gati yanaenda sambamba na miundombinu ya barabara ambapo alikiri kwasasa serikali ilishindwa kutenga fedha kwa ajili ya barabara ya Bungu-Nyamisati.
Alisema kwasasa wataiimarisha kwa kiwango cha changalawe ili iweze kutumika wakati wote licha ya hamu ya wilaya kutaka ijengwe kwa kiwango cha lami barabara hiyo.
Majaliwa alieleza kwa mwaka huu,wameendelea kulipa madeni ya barabara kuu ikiwemo Dar es salaam,Lindi,Masasi kwani mkandarasi alikuwa akidai fedha kutoka Masasi ,Tunduru,Namtumbo,Songea, Mbinga na Mbababei.

No comments:

Post a Comment