Rais Dkt. John Pombe Magufuli
akiwa katika picha ya pamoja na Spika wa Bunge, Job Ndugai, Mkewe Mama
Janet Magufuli, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi na Mawaziri
mara baada ya hafla ya uzindzi wa ndege mpya za abiria aina ya Bombadier
– 8 Q400 zilizonunuliwa na Serikali kutoka nchini
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John
Kijazi akiwekeana saini ya makabidhiano ya ndege mpya za abiria aina ya
Bombadier- 8 Q400 baina yake na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt. Leonard Chamuhilo wakati wa hafla ya
uzinduzi wa ndege hizo leo Jijini Dar es Salaam.
…………………………………………………..
Na. Sheila Simba MAELEZO Dar es Salaam
RAIS John Magufuli amesema
Serikali imejipanga kununua ndege mbili aina Jet zenye uwezo wa kubeba
abiria 160 na 242 pamoja na kutenga Tsh. Bilioni 100 kwa ajili ya
ukarabati viwanja vya ndege nchini.
Amesema hayo leo Jijini Dar Es
Salaam wakati wa uzinduzi wa ndege mpya mbili za abria aina ya
bombardier – 8 Q400 zilizonunuliwa na Serikali kutoka nchini Canada ,na
kuongeza kuwa ndege hizo zitasaidia kuboresha sekta ya usafiri wa anga
nchini.
“Ndege hizi ni nzuri sana, kwani
ukitaka kujenga nchi yenye uchumi wa kisasa huwezi kujenga bila kuwa na
ndege na ukitaka watalii lazima uwe na ndege” alisema Rais Magufuli
Alisema kuwa ndege hizo mbili
zitakazonunuliwa na Serikali zitakuwa na uwezo wa kubeba kusaidia
watalii kuja nchini moja kwa moja bila kutua nchi nyingine.
“Tunataka watalii wanaokuja
nchini kuja moja kwa moja bila kushuka nchi nyingine ili kuongeza mapato
yetu na kukuza utalii duniani na kuwa na ndege nyingi zaidi kama nchi
nyingine”,alisema Rais Magufuli
Akizungumzia ubora wa ndege za
bombardier alisema kuwa ndege hizo zinaenda na mazingira ya hapa nchini
na zina uwezo wa kutua katika viwanja vyenye lami na vile ambavyo havina
lami na uendeshaji wake ni wa gharama nafuu.
Kwa mujibu wa Rais Magufuli
alisema kuwa ndege za bombardier zinatumia mafuta kidogo ikiwemo gharama
ya tsh Milioni 1 za mafuta kwa safari moja ikilinganisha na ndege
nyingine zenye kutumia tsh. Milioni 28 kwa safari
Rais Magufuli aliitaka bodi ya
shirika la ndege Tanzania (ATCL) kufanya kazi nzuri ya kusimamia ndege
hizo na kutoa huduma nzuri na kuhakikisha wanapata faida ili serikali
waweze kununua ndege nyingi zaidi.
Alisema kuwa bodi ya ATCL wana
kazi kubwa ya kufanya kuboresha shirika hilo, kutokana na uzembe wa
wafanyakazi wake kutokuwa makini na kuwataka kupanga vizuri safari za
ngede hizo kwani zina uwezo wa kwenda mpaka nchi jirani.
“lazima mjue mnaingia kwenye
ushindani na washindani wenu hawawezi kufurahia wapo hujuma ili shirika
lisisonge mbele sasa fanyeni kazi”alisema Magufuli
Aidha amewaomba ATCL kutotumia
mawakala katika kukatisha tiketi na kuzingatia muda wa safari ulipangwa
na kutoa huduma nzuri kwa wateja wao ili kukuza utalii nchini na
kuwaomba watanzania kuwa wazalendo kwa kutumia usafiri huo.
Kwa upande wake Waziri wa
Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa alisema ndege hizo
zilizozinduliwa zinauwezo wa kubeba abiria 76 na abiria 6 wakiwa ni wa
daraja la biashara na 70 ni daraja la kawaida na ina uwezo wa kubeba
mzigo wa tani moja.
Ameongeza kuwa shirika la ATCL
lina upungufu mkubwa wa watalaamu katika maeneo mbalimbali ikiwemo,
marubani, wahandisi, wanasheria, maafisa biashara, wahasibu na
menejimenti na hatua inayosabisha shirika hilo kushindwa kujiendesha
vizuri.
Waziri Mbarawa alisema kuwa ATCL
wamejipanga kutoa huduma za usafiri katika viwanja vya Dodoma, Dar Es
Salaam Bukoba, Tabora, Zanzibar, Mbeya, Kilimanjaro, Mtwara, Mwanza
Kigoma, Arusha na Comoro.
No comments:
Post a Comment