Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa
ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa akitoa taarifa ya Pato la Taifa Robo
ya Pili (Aprili – Juni) ya Mwaka 2016 kwa waandishi wa habari leo
jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Kaimu Mkurugenzi wa Takwimu za
Uchumi wa ofisi hiyo Bi. Joy Sawe. Taarifa hiyo imeonyesha kuwa Pato la
Taifa limekua kwa kasi ya asilimia 7.9 katika kipindi cha mwezi Aprili
hadi Juni 2016 ikilinganishwa na kasi ya asilimia 5.8 katika kipindi
kama hicho mwaka 2015.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa
ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa akitoa taarifa ya Pato la Taifa Robo
ya Pili (Aprili – Juni) ya Mwaka 2016 kwa waandishi wa habari leo
jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Meneja wa Takwimu za Pato la Taifa
wa Ofisi hiyo Daniel Masolwa. Taarifa hiyo imeonyesha kuwa Pato la Taifa
limekua kwa kasi ya asilimia 7.9 katika kipindi cha mwezi Aprili hadi
Juni 2016 ikilinganishwa na kasi ya asilimia 5.8 katika kipindi kama
hicho mwaka 2015.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina
Chuwa (hayupo pichani) wakati akitoa taarifa ya Pato la Taifa Robo ya
Pili (Aprili – Juni) ya Mwaka 2016 leo jijini Dar es Salaam. Taarifa
hiyo imeonyesha kuwa Pato la Taifa limekua kwa kasi ya asilimia 7.9
katika kipindi cha mwezi Aprili hadi Juni 2016 ikilinganishwa na kasi ya
asilimia 5.8 katika kipindi kama hicho mwaka 2015. (PICHA NA EMMANUEL GHULA)
……………………………………………………………
Na Veronica Kazimoto-Dar es Salaam
Pato la Taifa limekua kwa jumla
ya thamani ya Shilingi trilioni 11.7 katika kipindi cha robo ya pili ya
mwaka 2016 ikilinganishwa na Shilingi trilioni 10.9 katika kipindi kama
hicho cha mwaka 2015.
Akizungumza na waandishi wa
habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi mkuu wa Ofisi ya Taifa ya
Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa amesema ukuaji wa pato la Taifa
umetokana na shughuli za kiuchumi ikiwemo kilimo, mifugo, misitu na
uvuvi ambapo shughuli hizo zimekuwa kwa asilimia 3.2 ikilinganishwa na
ukuaji wa asilimia 1.9 katika kipindi kama hicho mwaka 2015.
Kwa upande wa shughuli za
uchumi za viwanda na ujenzi, Dkt. Chuwa alisema kumekua na ongezeko la
asilimia 20.5 katika kipindi hicho ukilinganisha na ukuaji wa asilimia
11.2 mwaka 2015 katika shughuli za uchimbaji madini, mawe na kokoto.
Aidha shughuli za uzalishaji
bidhaa na viwanda zimeongeza kwa asilimia 9.1 katika kipindi cha robo ya
pili ya mwaka 2016 ukilinganisha na kasi ya asilimia 5.2 ya mwaka 2015.
Shughuli za uchukuzi na
uhifadhi, Dkt. Chuwa amesema kuwa shughuli hizo zimekua kwa kiwango cha
asilimia 30.6 zikisababishwa na usafirishaji wa abiria kwa njia ya reli
na barabara ikiwa ni pamoja na usafiri wa UDART.
Vilevile, shughuli za fedha na
bima zimeongezeka kwa kasi ya asilimia 12.5 ikilinganishwa na asilimia
10.0 iliyopatikana katika kipindi kama hicho mwaka 2015.
Dkt. Chuwa amefafanua kuwa
huduma za elimu zimekua kwa kasi ya asilimia 8.0 katika robo hiyo ya
mwaka ikilinganishwa na aslimia 7.4 ya kipindi kama hicho kwa mwaka 2015
ambapo ukuaji wa shughuli hii imetokana na ongezeko la wanafunzi
waliodahiliwa mwaka 2016.
Kwa upande wa Nchi za Afrika
Mashariki ambazo zimeshachambua na kutoa Pato la Taifa katika kipindi
kinachoishia Juni 2016 ni Rwanda ambapo Pato halisi la Nchi ya Rwanda
katika kipindi cha Aprili – Juni 2016 limeendelea kukua kwa asilimia 5.4
ikilinganisha na asilimia 7.2 ya miezi kama hiyo mwaka 2015.
No comments:
Post a Comment