NA HERIETH SEMGAZA
Wafanyabiashara katika soko la
kariakoo lililopo jijini Dares salaam wameombwa kuendelea kujitokeza kwa
wingi kuwachangia wahanga wa tetemeko la Bukoba mkoani Kagera leo
katika harambee iliyofanyika katikati ya soko la Kariakoo jijini Dar es
salaam
Hayo yamesemwa na Philimin Romano
Chonde Mwenyekiti wa wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Kariakoo(JWK) ambapo
alitaja jumla ya pesa na thamani ya vifaa mbalimbali vilivyochangwa
katika kampeni ya hiyo ,ambayo bado inaendelea amesema mpaka sasa
wamepokea Jumla ya shilingi milioni 60 laki saba na mia Tano
zimekuswanywa
Philimin Romano Chonde amesema tunaendelea kupokea mchango wenu
ili tuweze kuwasilisha kwa Waziri mkuu Mh. Kassim Majaliwa katika siku
itakayopangwa, Aidha amewapongeza wanachama,wafanyabiashara wote
waliojitokeza kutoa michango yao na kuwataka waendelee kujitoa katika
shughuri mbalimbali za Kitaifa.
Nae SILVER MANDE mhazini Wa JWK
amesema kuwa taasisi na wafanyabiashara wengine waendelee kujitokeza kwa
wingi ili kutoa michango yao na kufanikisha kazi hiyo ambayo ni muhimu
sana katika jamii yetu hasa kwa hawa wenzetu ambao walipata jamnga la
Tetemeko la Ardhi huko Bukoba na kuathiri maisha yao na shughuli zao za
kila siku.
Taasisi mbalimbali na wafanyabiashara tunaomba muwe mstari wa mbele kutoa michango na kwa yeyote atakaye kuwanacho alete ili tuweze kujumuisha rambirambi zetu na kuwasilisha kwa Mh. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
Taasisi mbalimbali na wafanyabiashara tunaomba muwe mstari wa mbele kutoa michango na kwa yeyote atakaye kuwanacho alete ili tuweze kujumuisha rambirambi zetu na kuwasilisha kwa Mh. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
No comments:
Post a Comment